Jeremiah 43:4 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Yohanani mwana wa Karea na makamanda wote wa majeshi pamoja na watu wote hawakutii aliyosema Mwenyezi-Mungu, kwamba wabaki katika nchi ya Yuda.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi Yohanani mwana wa Karea, na maafisa wote wa jeshi, na watu wote wakakataa kutii amri ya Mwenyezi Mungu ya kukaa katika nchi ya Yuda.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Yohana, mwana wa Karea, na wakuu wote wa majeshi, na watu wote hawakuitii sauti ya Bwana, kwamba wakae katika nchi ya Yuda.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Yohanani mwana wa Karea na makamanda wote wa majeshi pamoja na watu wote hawakutii aliyosema Mwenyezi-Mungu, kwamba wabaki katika nchi ya Yuda.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi Yohanani mwana wa Karea na maafisa wote wa jeshi na watu wote wakakataa kutii amri ya BWANA ya kukaa katika nchi ya Yuda.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi Yohanani mwana wa Karea, na maafisa wote wa jeshi, na watu wote wakakataa kutii amri ya bwana ya kukaa katika nchi ya Yuda.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi Yohana, mwana wa Karea, na wakuu wote wa majeshi, na watu wote hawakuitii sauti ya BWANA, kwamba wakae katika nchi ya Yuda.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, Yohanani mwana wa Karea na makamanda wote wa majeshi pamoja na watu wote hawakutii aliyosema Mwenyezi-Mungu, kwamba wabaki katika nchi ya Yuda.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Basi, Yohana, mwana wa Karea, nao wakuu wote wa vikosi nao watu wote wa ukoo huu hawakuisikia sauti ya Bwana, wakae katika nchi ya Yuda.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Yohana, mwana wa Karea, na wakuu wote wa majeshi, na watu wote hawakuitii sauti ya BWANA, kwamba wakae katika nchi ya Yuda.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, Yohana mwana wa Karea na wakubwa wote wa waaskari pamoja na watu wote hawakutii maneno ya Yawe, kwamba wabaki katika inchi ya Yuda.