Jeremiah 43:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo Yohanani mwana wa Karea na makamanda wote wa majeshi waliwachukua watu wote wa Yuda waliosalia ambao walikuwa wamerudi nchini Yuda kutoka mataifa yote ambako walikuwa wametawanywa;
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Badala yake, Yohanani mwana wa Karea na maafisa wote wa jeshi wakawaongoza mabaki yote ya Yuda waliokuwa wamerudi kuishi katika nchi ya Yuda kutoka mataifa yote ambayo walikuwa wametawanywa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini Yohana, mwana wa Karea, na wakuu wote wa majeshi, wakawatwaa wote waliosalia wa Yuda, waliokuwa wamerudi kutoka taifa zote walikofukuzwa, wakae katika Yuda;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo Yohanani mwana wa Karea na makamanda wote wa majeshi waliwachukua watu wote wa Yuda waliosalia ambao walikuwa wamerudi nchini Yuda kutoka mataifa yote ambako walikuwa wametawanywa;
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Badala yake, Yohanani mwana wa Karea na maafisa wote wa jeshi wakawaongoza mabaki yote ya Yuda waliokuwa wamerudi kuishi katika nchi ya Yuda kutoka katika mataifa yote ambayo walikuwa wametawanywa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Badala yake, Yohanani mwana wa Karea na maafisa wote wa jeshi wakawaongoza mabaki yote ya Yuda waliokuwa wamerudi kuishi katika nchi ya Yuda kutoka mataifa yote ambayo walikuwa wametawanywa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini Yohana, mwana wa Karea, na wakuu wote wa majeshi, wakawatwaa wote waliosalia wa Yuda, waliokuwa wamerudi kutoka mataifa yote walikofukuzwa, wakae katika Yuda;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hapo Yohanani mwana wa Karea na makamanda wote wa majeshi waliwachukua watu wote wa Yuda waliosalia ambao walikuwa wamerudi nchini Yuda kutoka mataifa yote ambako walikuwa wametawanywa;
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yohana, mwana wa Karea, na wakuu wote wa vikosi wakayachukua masao yote ya Wayuda waliorudi kukaa katika nchi ya Yuda wakitoka kwa mataifa yote, walikotupiwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini Yohana, mwana wa Karea, na wakuu wote wa majeshi, wakawatwaa wote waliosalia wa Yuda, waliokuwa wamerudi kutoka taifa zote walikofukuzwa, wakae katika Yuda;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu Yohana mwana wa Karea na wakubwa wote wa waaskari waliwapeleka watu wote wa Yuda waliobaki ambao walikuwa wamerudi katika inchi ya Yuda kutoka katika mataifa yote ambako walikuwa wamesambazwa: