Jeremiah 44:19 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nao wanawake wakasema, “Tulimfukizia ubani na kummiminia kinywaji malkia wa mbinguni. Tulifanya hivyo kwa kibali cha waume zetu. Tena tulimtengenezea mikate yenye sura yake na kummiminia kinywaji!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wanawake wakaongeza kusema, “Tulipomfukizia uvumba Malkia wa Mbinguni, na kummiminia sadaka zetu za kinywaji, je, waume zetu hawakujua kwamba tulikuwa tukitengeneza maandazi kwa mfano wake, na kummiminia yeye sadaka za kinywaji?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nasi tulipomfukizia uvumba malkia wa mbinguni, na kummiminia sadaka za kinywaji, je! Tulimfanyizia mikate, ili kumwabudu, na kummiminia mamiminiko, waume zetu wasipokuwapo?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nao wanawake wakasema, “Tulimfukizia ubani na kummiminia kinywaji malkia wa mbinguni. Tulifanya hivyo kwa kibali cha waume zetu. Tena tulimtengenezea mikate yenye sura yake na kummiminia kinywaji!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wanawake wakaongeza kusema, “Wakati tulipomfukizia uvumba Malkia wa Mbingu na kummiminia sadaka zetu za kinywaji, je, waume zetu hawakujua kwamba tulikuwa tukitengeneza maandazi kwa mfano wake na kummiminia yeye sadaka za kinywaji?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wanawake wakaongeza kusema, “Wakati tulipomfukizia uvumba Malkia wa Mbinguni na kummiminia sadaka zetu za kinywaji, je, waume zetu hawakujua kwamba tulikuwa tukitengeneza maandazi kwa mfano wake, na kummiminia yeye sadaka za kinywaji?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nasi tulipomfukizia uvumba malkia wa mbinguni, na kummiminia sadaka za kinywaji, je! Tulimwandalia mikate, ili kumwabudu, na kummiminia mimiminiko, waume zetu wasipokuwapo?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nao wanawake wakasema, “Tulimfukizia ubani na kummiminia kinywaji malkia wa mbinguni. Tulifanya hivyo kwa kibali cha waume zetu. Tena tulimtengenezea mikate yenye sura yake na kummiminia kinywaji!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena tukimvukizia mfalme wa kike wa mbinguni na kummwagia vinywaji vya tambiko, je? Waume wetu hawako, tukimtengenezea mikate yenye mifano yake na kummwagia vinywaji vya tambiko?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nasi tulipomfukizia uvumba malkia wa mbinguni, na kummiminia sadaka za kinywaji, je! Tulimfanyizia mikate, ili kumwabudu, na kummiminia mamiminiko, waume zetu wasipokuwapo?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nao wanawake wakasema: Tulimufukizia malkia wa mbinguni ubani na kumutolea sadaka ya kinywaji. Tulifanya hivyo kwa ruhusa ya waume wetu. Tena tulimutengenezea mikate yenye sura yake na kumutolea sadaka ya kinywaji.