Jeremiah 44:22 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu hakuweza kuvumilia tena matendo yenu maovu na mambo ya kuchukiza mliyotenda; ndiyo maana nchi yenu imekuwa ukiwa, jangwa, laana na bila wakazi, kama ilivyo mpaka leo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwenyezi Mungu alipokuwa hawezi kuendelea kuvumilia matendo yenu maovu na mambo ya machukizo mliyoyafanya, nchi yenu ilikuwa kitu cha kulaaniwa na kuachwa ukiwa pasipo wakazi, kama ilivyo leo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata Bwana asiweze kuvumilia tena, kwa sababu ya uovu wa matendo yenu, na kwa sababu ya machukizo mliyoyafanya; kwa sababu hiyo nchi yenu imekuwa ukiwa, na ajabu, na laana, isikaliwe na mtu kama ilivyo leo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu hakuweza kuvumilia tena matendo yenu maovu na mambo ya kuchukiza mliyotenda; ndiyo maana nchi yenu imekuwa ukiwa, jangwa, laana na bila wakazi, kama ilivyo mpaka leo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
BWANA alipokuwa hawezi kuendelea kuvumilia matendo yenu maovu na mambo ya machukizo mliyoyafanya, nchi yenu ilikuwa kitu cha kulaania na kuachwa ukiwa pasipo wakazi, kama ilivyo leo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
bwana alipokuwa hawezi kuendelea kuvumilia matendo yenu maovu na mambo ya machukizo mliyoyafanya, nchi yenu ilikuwa kitu cha kulaania na kuachwa ukiwa pasipo wakazi, kama ilivyo leo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hata BWANA asiweze kuvumilia tena, kwa sababu ya uovu wa matendo yenu, na kwa sababu ya machukizo mliyoyafanya; kwa sababu hiyo nchi yenu imekuwa ukiwa, na ajabu, na laana, isikaliwe na mtu kama ilivyo leo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu hakuweza kuvumilia tena matendo yenu maovu na mambo ya kuchukiza mliyotenda; ndiyo maana nchi yenu imekuwa ukiwa, jangwa, laana na bila wakazi, kama ilivyo mpaka leo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo Bwana hakuweza kuvumilia tena kwa ajili ya ubaya wa matendo yenu na kwa ajili ya matapisho, mliyoyafanya; ndipo, nchi ilipogeuka kuwa mavunjiko na mapori tu, ikaapizwa, pasiwepo aikaaye, kama ilivyo siku hizi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata BWANA asiweze kuvumilia tena, kwa sababu ya uovu wa matendo yenu, na kwa sababu ya machukizo mliyoyafanya; kwa sababu hiyo nchi yenu imekuwa ukiwa, na ajabu, na laana, isikaliwe na mtu kama ilivyo leo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe hakuweza kuvumilia tena matendo yenu maovu na mambo ya kuchukiza muliyotenda; ndiyo maana inchi yenu imekuwa ukiwa, jangwa, laana na bila wakaaji, kama inavyokuwa mpaka leo.