Jeremiah 44:26 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini sikilizeni neno langu mimi Mwenyezi-Mungu, enyi watu wote wa Yuda mnaokaa nchini Misri. Mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Naapa kwa jina langu kuu kwamba hakuna mtu yeyote wa Yuda katika nchi yote ya Misri atakayelitumia jina langu kuapa nalo akisema: ‘Kama aishivyo Bwana Mwenyezi-Mungu!’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini sikieni neno la Mwenyezi Mungu, enyi Wayahudi wote mnaoishi Misri: ‘Ninaapa kwa Jina langu lililo kuu,’ asema Mwenyezi Mungu, ‘kwamba hakuna hata mmoja atokaye Yuda anayeishi popote Misri ambaye kamwe ataomba tena kwa Jina langu au kuapa, akisema, “Hakika kama Bwana Mungu Mwenyezi aishivyo.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, kwa sababu hiyo lisikieni neno la Bwana, ninyi nyote wa Yuda, mnaokaa katika nchi ya Misri, Tazama, nimeapa kwa jina langu kuu, asema Bwana, ya kwamba jina langu halitatajwa tena katika kinywa cha mtu awaye yote wa Yuda, katika nchi yote ya Misri, akisema, Kama Bwana MUNGU aishivyo!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini sikilizeni neno langu mimi Mwenyezi-Mungu, enyi watu wote wa Yuda mnaokaa nchini Misri. Mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Naapa kwa jina langu kuu kwamba hakuna mtu yeyote wa Yuda katika nchi yote ya Misri atakayelitumia jina langu kuapa nalo akisema: ‘Kama aishivyo Bwana Mwenyezi-Mungu!’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini sikieni neno la BWANA, enyi Wayahudi wote mnaoishi Misri: ‘Ninaapa kwa Jina langu lililo kuu,’ asema BWANA, ‘kwamba hakuna hata mmoja atokaye Yuda anayeishi po pote katika Misri ambaye kamwe ataomba tena kwa Jina langu au kuapa, akisema, “Hakika kama BWANA Mwenyezi aishivyo.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini sikieni neno la bwana, enyi Wayahudi wote mnaoishi Misri: ‘Ninaapa kwa Jina langu lililo kuu,’ asema bwana, ‘kwamba hakuna hata mmoja atokaye Yuda anayeishi popote Misri ambaye kamwe ataomba tena kwa Jina langu au kuapa, akisema, “Hakika kama bwana Mwenyezi aishivyo.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, kwa sababu hiyo lisikieni neno la BWANA, ninyi nyote wa Yuda, mnaokaa katika nchi ya Misri, Tazama, nimeapa kwa jina langu kuu, asema BWANA, ya kwamba jina langu halitatajwa tena katika kinywa cha mtu awaye yote wa Yuda, katika nchi yote ya Misri, akisema, Kama Bwana MUNGU aishivyo!
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini sikilizeni neno langu mimi Mwenyezi-Mungu, enyi watu wote wa Yuda mnaokaa nchini Misri. Mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Naapa kwa jina langu kuu kwamba hakuna mtu yeyote wa Yuda katika nchi yote ya Misri atakayelitumia jina langu kuapa nalo akisema: ‘Kama aishivyo Bwana Mwenyezi-Mungu!’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini lisikieni neno la Bwana, ninyi Wayuda wote mkaao katika nchi ya Misri! Bwana anasema: Tazameni, nimeapa katika Jina langu kubwa kwamba: Jina langu lisitajwe tena katika nchi yote ya Misri vinywani mwa watu wa Kiyuda wo wote wakisema: Hivyo, Bwana Mungu alivyo Mwenye uzima!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, kwa sababu hiyo lisikieni neno la BWANA, ninyi nyote wa Yuda, mnaokaa katika nchi ya Misri, Tazama, nimeapa kwa jina langu kuu, asema BWANA, ya kwamba jina langu halitatajwa tena katika kinywa cha mtu awaye yote wa Yuda, katika nchi yote ya Misri, akisema, Kama Bwana MUNGU aishivyo!
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini musikilize neno la Yawe, enyi watu wote wa Yuda munaokaa katika inchi ya Misri. Yawe anasema hivi: Ninaapa kwa jina langu kubwa kwamba hakuna mutu yeyote wa Yuda katika inchi yote ya Misri atakayelitumia jina langu kwa kuapa nalo akisema: Kama vile Bwana wangu Yawe anavyoishi.