Jeremiah 44:28 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ni wachache watakaonusurika vitani na kurudi kutoka nchi ya Misri na kwenda nchini Yuda. Hapo watu wa Yuda wote waliobaki kati ya wale waliokwenda kukaa Misri watatambua ni tamko la nani lenye nguvu: Langu au lao!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wale watakaonusurika upanga na kurudi katika nchi ya Yuda kutoka Misri watakuwa wachache sana. Ndipo mabaki wote wa Yuda waliokuja kuishi Misri watajua ni neno la nani litakalosimama: kwamba ni langu au ni lao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao watakaoukimbia upanga, watatoka katika nchi ya Misri, na kuiingia nchi ya Yuda, watu wachache sana; na wote wa Yuda waliosalia, waliokwenda nchi ya Misri ili kukaa huko, watajua ni neno la nani litakalosimama, neno langu, au neno lao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ni wachache watakaonusurika vitani na kurudi kutoka nchi ya Misri na kwenda nchini Yuda. Hapo watu wa Yuda wote waliobaki kati ya wale waliokwenda kukaa Misri watatambua ni tamko la nani lenye nguvu: langu au lao!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wale watakaonusurika upanga na kurudi katika nchi ya Yuda kutoka Misri watakuwa wachache sana. Ndipo mabaki wote wa Yuda waliokuja kuishi Misri watakapojua ni neno la nani litakalosimama, kwamba ni langu au lao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wale watakaonusurika upanga na kurudi katika nchi ya Yuda kutoka Misri watakuwa wachache sana. Ndipo mabaki wote wa Yuda waliokuja kuishi Misri watakapojua ni neno la nani litakalosimama, kwamba ni langu au lao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao watakaoukimbia upanga, watatoka katika nchi ya Misri, na kuiingia katika nchi ya Yuda, watu wachache sana; na wote wa Yuda waliosalia, waliokwenda katika nchi ya Misri ili kukaa huko, watajua ni neno la nani litakalosimama, neno langu, au neno lao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ni wachache watakaonusurika vitani na kurudi kutoka nchi ya Misri na kwenda nchini Yuda. Hapo watu wa Yuda wote waliobaki kati ya wale waliokwenda kukaa Misri watatambua ni tamko la nani lenye nguvu: Langu au lao!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao watakaopona panga watatoka katika nchi ya Misri, warudi katika nchi ya Yuda, lakini watakuwa wachache sana, mkiwahesabu. Ndipo, masao yote ya Yuda waliokuja Misri kukaa ugenini huku watakapojua, kama ni neno lipi litakalosimama, langu au lao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao watakaoukimbia upanga, watatoka katika nchi ya Misri, na kuiingia nchi ya Yuda, watu wachache sana; na wote wa Yuda waliosalia, waliokwenda nchi ya Misri ili kukaa huko, watajua ni neno la nani litakalosimama, neno langu, au neno lao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ni wachache tu ndio watakaoponyoka katika vita na kurudi kutoka inchi ya Misri na kwenda katika inchi ya Yuda. Halafu Wayuda wote waliobaki kati ya wale waliokwenda kukaa Misri watatambua ni neno la nani lenye nguvu: langu au lao!