Jeremiah 44:7 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Sasa, mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, nauliza hivi: Mbona mnajiletea madhara makubwa namna hii, na kujiangamiza nyinyi wenyewe, wanaume kwa wanawake, watoto wadogo na wachanga, hata pasibaki mtu katika Yuda?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Basi hili ndilo Bwana Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu wa Israeli, asemalo: Kwa nini kujiletea maafa makubwa kama haya juu yenu kwa kujikatilia mbali kutoka Yuda wanaume na wanawake, watoto na wanyonyao, hata kujiacha bila mabaki?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, sasa, Bwana, Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Kwa nini mnafanya uovu huu mkubwa juu ya nafsi zenu wenyewe, kujikatilia mbali mwanamume na mwanamke, mtoto mchanga na anyonyaye, mtoke kati ya Yuda, msijiachie mtu abakiye;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Sasa, mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, nauliza hivi: Mbona mnajiletea madhara makubwa namna hii, na kujiangamiza nyinyi wenyewe, wanaume kwa wanawake, watoto wadogo na wachanga, hata pasibaki mtu katika Yuda?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Basi hili ndilo BWANA Mungu Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: Kwa nini kujiletea maafa makubwa kama haya juu yenu kwa kujikatilia mbali mtoke Yuda wanaume na wanawake, watoto na wanyonyao hata kujiacha bila mabaki?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Basi hili ndilo bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: Kwa nini kujiletea maafa makubwa kama haya juu yenu kwa kujikatilia mbali kutoka Yuda wanaume na wanawake, watoto na wanyonyao, hata kujiacha bila mabaki?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, sasa, BWANA, Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Kwa nini mnafanya uovu huu mkubwa juu ya nafsi zenu wenyewe, kujikatilia mbali mwanamume na mwanamke, mtoto mchanga na anyonyaye, mtoke kati ya Yuda, msijiachie mtu abakiye;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Sasa, mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, nauliza hivi: Mbona mnajiletea madhara makubwa namna hii, na kujiangamiza nyinyi wenyewe, wanaume kwa wanawake, watoto wadogo na wachanga, hata pasibaki mtu katika Yuda?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sasa hivi ndivyo, Bwana Mungu Mwenye vikosi, Mungu wa Isiraeli, anavyosema: Mbona mnazifanyizia roho zenu mabaya makuu, mwang'oe kwenu waume na wake, vijana na wachanga, watoweke katikati ya Wayuda, kwenu lisisalie hata sao?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, sasa, BWANA, Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Kwa nini mnafanya uovu huu mkubwa juu ya nafsi zenu wenyewe, kujikatilia mbali mwanamume na mwanamke, mtoto mchanga na anyonyaye, mtoke kati ya Yuda, msijiachie mtu abakiye;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sasa, Yawe wa majeshi, Mungu wa Israeli anasema hivi: Mbona munajiletea maovu makubwa namna hii, na kujiangamiza ninyi wenyewe, wanaume kama vile wanawake, watoto wadogo na wachanga, hata kusibaki mutu katika inchi ya Yuda?