Jeremiah 44:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Je, mmesahau uovu wa wazee wenu, uovu wa wafalme wa Yuda, uovu wa wake zao na uovu wenu nyinyi wenyewe na wa wake zenu, ambao mliufanya nchini Yuda na kwenye barabara za Yerusalemu?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Je, mmesahau uovu uliotendwa na baba zenu, na wafalme na malkia wa Yuda, na uovu uliofanywa na ninyi na wake zenu katika nchi ya Yuda na barabara za Yerusalemu?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Je! Mmeusahau uovu wa baba zenu, na uovu wa wafalme wa Yuda, na uovu wa wake zao, na uovu wenu wenyewe, na uovu wa wake zenu, walioutenda katika nchi ya Yuda, na katika njia kuu za Yerusalemu?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Je, mmesahau uovu wa wazee wenu, uovu wa wafalme wa Yuda, uovu wa wake zao na uovu wenu nyinyi wenyewe na wa wake zenu, ambao mliufanya nchini Yuda na kwenye barabara za Yerusalemu?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Je, mmesahau uovu uliotendwa na baba zenu na wafalme na malkia wa Yuda na uovu uliofanywa na ninyi na wake zenu katika nchi ya Yuda na barabara za Yerusalemu?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Je, mmesahau uovu uliotendwa na baba zenu, na wafalme na malkia wa Yuda, na uovu uliofanywa na ninyi na wake zenu katika nchi ya Yuda na barabara za Yerusalemu?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Je! Mmeusahau uovu wa baba zenu, na uovu wa wafalme wa Yuda, na uovu wa wake zao, na uovu wenu wenyewe, na uovu wa wake zenu, walioutenda katika nchi ya Yuda, na katika njia kuu za Yerusalemu?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Je, mmesahau uovu wa wazee wenu, uovu wa wafalme wa Yuda, uovu wa wake zao na uovu wenu nyinyi wenyewe na wa wake zenu, ambao mliufanya nchini Yuda na kwenye barabara za Yerusalemu?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Je? Mmeyasahau mabaya ya baba zenu na mabaya ya wafalme wa Yuda na mabaya ya wake zao na mabaya yenu na mabaya ya wake zenu, waliyoyafanya katika nchi ya Yuda namo barabarani mwa Yerusalemu?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Je! Mmeusahau uovu wa baba zenu, na uovu wa wafalme wa Yuda, na uovu wa wake zao, na uovu wenu wenyewe, na uovu wa wake zenu, walioutenda katika nchi ya Yuda, na katika njia kuu za Yerusalemu?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mumesahau uovu wa babu zenu, uovu wa wafalme wa Yuda, uovu wa wake wao na uovu wenu ninyi wenyewe na wa wake wenu, ambao muliufanya katika inchi ya Yuda na kwenye barabara za Yerusalema?