Jeremiah 45:4 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini Mwenyezi-Mungu ameniambia nikuambie hivi: Tazama, yale niliyojenga nayabomoa, na yale niliyopanda nayangoa; nitafanya hivyo katika nchi yote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini Mwenyezi Mungu akasema, “Mwambie hivi: ‘Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: Nitakibomoa kile nilichokijenga, na kung’oa kile nilichokipanda katika nchi yote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, mwambie hivi, Bwana asema hivi, Tazama, niliyoyajenga nitayabomoa, na niliyoyapanda nitayang'oa; na haya yatakuwa katika nchi yote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini Mwenyezi-Mungu ameniambia nikuambie hivi: Tazama, yale niliyojenga nayabomoa, na yale niliyopanda nayang'oa; nitafanya hivyo katika nchi yote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
BWANA akasema, “Mwambie hivi: ‘Hili ndilo asemalo BWANA: Nitakibomoa kile nilichokijenga na kung'oa kile nilichokipanda, katika nchi yote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
bwana akasema, “Mwambie hivi: ‘Hili ndilo asemalo bwana: Nitakibomoa kile nilichokijenga, na kung’oa kile nilichokipanda katika nchi yote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, mwambie hivi, BWANA asema hivi, Tazama, niliyoyajenga nitayabomoa, na niliyoyapanda nitayang'oa; na haya yatakuwa katika nchi yote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini Mwenyezi-Mungu ameniambia nikuambie hivi: Tazama, yale niliyojenga nayabomoa, na yale niliyopanda nayangoa; nitafanya hivyo katika nchi yote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Utamwambia hivyo: Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Unaniona mimi, ninavyoyabomoa, niliyoyajenga, ninavyoyang'oa, niliyoyapanda! Vinakuwa hivyo katika nchi yote nzima.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, mwambie hivi, BWANA asema hivi, Tazama, niliyoyajenga nitayabomoa, na niliyoyapanda nitayang’oa; na haya yatakuwa katika nchi yote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Yawe ameniambia nikuambie: Yawe anasema hivi: Yale niliyojenga ninayabomoa, na yale niliyopanda ninayaongoa; nitafanya hivyo katika inchi yote.