Jeremiah 46:10 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Siku hiyo ni siku ya Mwenyezi-Mungu wa majeshi, ni siku ya kulipiza kisasi; naam, siku ya kuwaadhibu maadui zake. Upanga utawamaliza hao na kutosheka, utainywa damu yao na kushiba. Maana Mwenyezi-Mungu wa majeshi anayo kafara huko kaskazini karibu na mto Eufrate.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini ile siku ni ya Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, siku ya kulipiza kisasi, kisasi juu ya adui zake. Upanga utakula hata utakapotosheka, hadi utakapozima kiu yake kwa damu. Kwa maana Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, atatoa dhabihu kwenye nchi ya kaskazini, kando ya Mto Frati.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana hiyo ni siku ya Bwana, Bwana wa majeshi, Siku ya kisasi, ili ajilipize kisasi juu ya adui zake; Nao upanga utakula na kushiba, Utakunywa damu yao hata kukinai; Maana Bwana, Bwana wa majeshi, ana sadaka yake Katika nchi ya kaskazini karibu na mto Frati.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Siku hiyo ni siku ya Mwenyezi-Mungu wa majeshi, ni siku ya kulipiza kisasi; naam, siku ya kuwaadhibu maadui zake. Upanga utawamaliza hao na kutosheka, utainywa damu yao na kushiba. Maana Mwenyezi-Mungu wa majeshi anayo kafara huko kaskazini karibu na mto Eufrate.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini ile siku ni ya Bwana, BWANA Mwenye Nguvu Zote, siku ya kulipiza kisasi, kisasi juu ya adui zake. Upanga utakula mpaka utakapotosheka, mpaka utakapozima kiu yake kwa damu. Kwa maana Bwana, BWANA Mwenye Nguvu Zote, atatoa dhabihu kwenye nchi ya kaskazini, kando ya Mto Eufrati.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini ile siku ni ya Bwana, bwana Mwenye Nguvu Zote, siku ya kulipiza kisasi, kisasi juu ya adui zake. Upanga utakula hata utakapotosheka, hadi utakapozima kiu yake kwa damu. Kwa maana Bwana, bwana Mwenye Nguvu Zote, atatoa dhabihu kwenye nchi ya kaskazini, kando ya Mto Frati.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana hiyo ni siku ya Bwana, BWANA wa majeshi, Siku ya kisasi, ili ajilipize kisasi juu ya adui zake; Nao upanga utakula na kushiba, Utakunywa damu yao hata kukinai; Maana Bwana, BWANA wa majeshi, ana sadaka yake Katika nchi ya kaskazini karibu na mto Frati.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Siku hiyo ni siku ya Mwenyezi-Mungu wa majeshi, ni siku ya kulipiza kisasi; naam, siku ya kuwaadhibu maadui zake. Upanga utawamaliza hao na kutosheka, utainywa damu yao na kushiba. Maana Mwenyezi-Mungu wa majeshi anayo kafara huko kaskazini karibu na mto Eufrate.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku hii ni yake Bwana Mungu Mwenye vikosi, ni siku ya lipizi ya kuwalipiza wapingani wake, panga zitakula, zishibe, mpaka zilewe kwa damu zao, kwani wao ndio kama ng'ombe za kumtambikia Bwana Mungu Mwenye vikosi katika nchi ya upande wa kaskazini kwenye mto wa Furati.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana hiyo ni siku ya Bwana, BWANA wa majeshi, Siku ya kisasi, ili ajilipize kisasi juu ya adui zake; Nao upanga utakula na kushiba, Utakunywa damu yao hata kukinai; Maana Bwana, BWANA wa majeshi, ana sadaka yake Katika nchi ya kaskazini karibu na mto Frati.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini siku hiyo ni siku ya Bwana wetu Yawe wa majeshi. Ni siku ya kulipiza kisasi, siku ya kuwaazibu waadui zake. Upanga utawamaliza hao na kutosheka, utaikunywa damu yao na kushiba. Maana Bwana wetu Yawe wa majeshi yuko na sadaka huko kaskazini karibu na muto Furati.