Jeremiah 46:18 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mimi naapa kwa uhai wangu nasema mimi mfalme niitwaye Mwenyezi-Mungu wa majeshi, kweli adui anakuja kuwashambulieni: Ni hakika kama Tabori ulivyo mlima kama mlima Karmeli uonekanavyo kutoka baharini.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Kwa hakika kama niishivyo,” asema Mfalme, ambaye jina lake ni Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, “mmoja atakuja ambaye ni kama Tabori miongoni mwa milima, kama Karmeli kando ya bahari.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kama mimi niishivyo, asema Mfalme, ambaye jina lake ni Bwana wa majeshi, hakika yake, kama Tabori katika milima, na kama Karmeli karibu na bahari, ndivyo atakavyokuja.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mimi naapa kwa uhai wangu nasema mimi mfalme niitwaye Mwenyezi-Mungu wa majeshi, kweli adui anakuja kuwashambulieni: ni hakika kama Tabori ulivyo mlima kama mlima Karmeli uonekanavyo kutoka baharini.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Kwa hakika kama niishivyo,” asema Mfalme, ambaye jina lake ni BWANA Mwenye Nguvu Zote, “mmoja atakuja ambaye ni kama Tabori miongoni mwa milima, kama Karmeli kando ya bahari.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Kwa hakika kama niishivyo,” asema Mfalme, ambaye jina lake ni bwana Mwenye Nguvu Zote, “mmoja atakuja ambaye ni kama Tabori miongoni mwa milima, kama Karmeli kando ya bahari.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kama mimi niishivyo, asema Mfalme, ambaye jina lake ni BWANA wa majeshi, hakika yake, kama Tabori katika milima, na kama Karmeli karibu na bahari, ndivyo atakavyokuja.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mimi naapa kwa uhai wangu nasema mimi mfalme niitwaye Mwenyezi-Mungu wa majeshi, kweli adui anakuja kuwashambulieni: Ni hakika kama Tabori ulivyo mlima kama mlima Karmeli uonekanavyo kutoka baharini.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndivyo, asemavyo Mfalme, Jina lake Bwana Mwenye vikosi: Hivyo, nilivyo Mwenye uzima, atakuja afananaye na Tabori ulio mkuu wa kuipita milima mingine au na Karmeli huko pwani.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kama mimi niishivyo, asema Mfalme, ambaye jina lake ni BWANA wa majeshi, hakika yake, kama Tabori katika milima, na kama Karmeli karibu na bahari, ndivyo atakavyokuja.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kama vile ninavyoishi, –ni ujumbe wa mufalme, jina lake Yawe wa majeshi– kweli adui anakuja kuwashambulia: ni hakika kama vile Tabori unavyokuwa mulima, kama vile mulima Karmeli unavyoonekana kutoka katika bahari.