Jeremiah 46:25 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, alisema: “Tazama, mimi nitamwadhibu Amoni mungu wa Thebesi, nitaiadhibu Misri na miungu yake na wafalme wake, nitamwadhibu Farao na wote wanaomtegemea.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu wa Israeli, asema: “Ninakaribia kuleta adhabu juu ya Amoni mungu wa Thebesi, na juu ya Farao, juu ya Misri na miungu yake, na wafalme wake, pamoja na wanaomtegemea Farao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Tazama, nitamwadhibu Amoni wa No, na Farao, na Misri, pamoja na miungu yake, na wafalme wake, naam, Farao, na hao wanaomtumainia;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, alisema: “Tazama, mimi nitamwadhibu Amoni mungu wa Thebesi, nitaiadhibu Misri na miungu yake na wafalme wake, nitamwadhibu Farao na wote wanaomtegemea.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
BWANA Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asema: “Nakaribia kuleta adhabu juu ya Amoni mungu wa Thebesi, na juu ya Farao, Misri na miungu yake, wafalme wake pamoja na wale wanaomtegemea Farao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asema: “Nakaribia kuleta adhabu juu ya Amoni mungu wa Thebesi, na juu ya Farao, Misri na miungu yake, na wafalme wake, pamoja na wale wanaomtegemea Farao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Tazama, nitamwadhibu Amoni wa Tebesi, na Farao, na Misri, pamoja na miungu yake, na wafalme wake, naam, Farao, na hao wanaomtumainia;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, alisema: “Tazama, mimi nitamwadhibu Amoni mungu wa Thebesi, nitaiadhibu Misri na miungu yake na wafalme wake, nitamwadhibu Farao na wote wanaomtegemea.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Bwana Mwenye vikosi, Mungu wa Isiraeli, anasema: Mtaniona, ninavyompatiliza Amoni wa No naye Farao na nchi yake ya Misri hata miungu yake na wafalme wake; nitampatiliza Farao kweli nao wote wamwegemeao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Tazama, nitamwadhibu Amoni wa No, na Farao, na Misri, pamoja na miungu yake, na wafalme wake, naam, Farao, na hao wanaomtumainia;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe wa majeshi, Mungu wa Israeli, alisema: Mimi nitamwazibu Amoni mungu wa muji wa Tebesi, nitaiazibu Misri na miungu yake na wafalme wake, nitamwazibu Mufalme wa Misri na wote wanaomutegemea.