Jeremiah 46:26 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nitawatia mikononi mwa wale wanaotaka kuyaangamiza maisha yao, yaani Nebukadneza mfalme wa Babuloni na maofisa wake. Baadaye, nchi ya Misri itakaliwa na watu kama ilivyokuwa hapo zamani. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nitawatia mikononi mwa wanaoutafuta uhai wao, yaani Nebukadneza mfalme wa Babeli na maafisa wake. Mwishowe, hata hivyo, Misri itakaliwa kama nyakati zilizopita,” asema Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
nami nitawatia katika mikono ya hao wanaowatafuta roho zao, na katika mikono ya Nebukadreza, mfalme wa Babeli, na katika mikono ya watumishi wake; na baada ya hayo itakaliwa na watu, kama katika siku za kale, asema Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nitawatia mikononi mwa wale wanaotaka kuyaangamiza maisha yao, yaani Nebukadneza mfalme wa Babuloni na maofisa wake. Baadaye, nchi ya Misri itakaliwa na watu kama ilivyokuwa hapo zamani. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nitawatia mikononi mwa wale wanaotafuta uhai wao, yaani Nebukadneza mfalme wa Babeli na maafisa wake. Hatimaye, hata hivyo, Misri itakaliwa kama nyakati zilizopita,” asema BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nitawatia mikononi mwa wale wanaotafuta uhai wao, yaani Nebukadneza mfalme wa Babeli na maafisa wake. Hatimaye, hata hivyo, Misri itakaliwa kama nyakati zilizopita,” asema bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
nami nitawatia katika mikono ya hao wanaowatafuta roho zao, na katika mikono ya Nebukadneza, mfalme wa Babeli, na katika mikono ya watumishi wake; na baada ya hayo itakaliwa na watu, kama katika siku za kale, asema BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nitawatia mikononi mwa wale wanaotaka kuyaangamiza maisha yao, yaani Nebukadneza mfalme wa Babuloni na maofisa wake. Baadaye, nchi ya Misri itakaliwa na watu kama ilivyokuwa hapo zamani. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nitawatia mikononi mwao wanaozitafuta roho zao, namo mikononi mwa Nebukadinesari, mfalme wa Babeli, namo mikononi mwa watumishi wake. Lakini hayo yatakapokwisha, nchi itakaa watu kama siku za kale; ndivyo, asemavyo Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
nami nitawatia katika mikono ya hao wanaowatafuta roho zao, na katika mikono ya Nebukadreza, mfalme wa Babeli, na katika mikono ya watumishi wake; na baada ya hayo itakaliwa na watu, kama katika siku za kale, asema BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nitawatia katika mikono ya wale wanaotaka kuyaangamiza maisha yao, ni kusema Nebukadneza mufalme wa Babeli na wakubwa wake. Kisha, inchi ya Misri itakaliwa na watu kama ilivyokuwa hapo zamani. –Ni ujumbe wa Yawe.