Jeremiah 46:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Songeni mbele, enyi farasi, shambulieni enyi magari ya farasi. Mashujaa wasonge mbele: Watu wa Kushi na Puti washikao ngao, watu wa Ludi, stadi wa kutumia pinde.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Songeni mbele, enyi farasi! Endesheni kwa kasi, enyi mnaoendesha magari ya vita! Endeleeni mbele, enyi mashujaa: wanaume wa Kushi na Putu mnaobeba ngao, wanaume wa Ludi mnaovuta upinde.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Haya! Pandeni, enyi farasi; Jihimizeni, enyi magari ya vita; Mashujaa nao na watoke nje Kushi na Puti, watumiao ngao; Nao Waludi, washikao uta na kuupeta.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Songeni mbele, enyi farasi, shambulieni enyi magari ya farasi. Mashujaa wasonge mbele: watu wa Kushi na Puti washikao ngao, watu wa Ludi, stadi wa kutumia pinde.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Songeni mbele, Enyi farasi! Endesheni kwa ukali, Enyi magari ya farasi, Endeleeni mbele, Enyi mashujaa: watu wa Kushi na Putu wachukuao ngao, watu wa Ludi wavutao upinde.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Songeni mbele, enyi farasi! Endesheni kwa ukali, enyi magari ya farasi, Endeleeni mbele, enyi mashujaa: watu wa Kushi na Putu wachukuao ngao, watu wa Ludi wavutao upinde.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Haya! Pandeni, enyi farasi; Jihimizeni, enyi magari ya vita; Mashujaa nao na watoke nje Kushi na Puti, watumiao ngao; Nao Waludi, washikao uta na kuupinda.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Songeni mbele, enyi farasi, shambulieni enyi magari ya farasi. Mashujaa wasonge mbele: Watu wa Kushi na Puti washikao ngao, watu wa Ludi, stadi wa kutumia pinde.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Pandeni, ninyi farasi! Pigeni mbio kama wenye wazimu, ninyi magari! Wapiga vita na watokee, wale Wanubi na Waputi washikao ngao na Waludi washikao pindi, wajuao kuzivuta!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Haya! Pandeni, enyi farasi; Jihimizeni, enyi magari ya vita; Mashujaa nao na watoke nje Kushi na Puti, watumiao ngao; Nao Waludi, washikao uta na kuupeta.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Musonge mbele, enyi farasi; mushambulie, enyi magari ya vita. Mashujaa wasonge mbele: watu wa Etiopia na Puti wanaoshika ngao, watu wa Ludi, wafundi wa kutumia pinde.