Jeremiah 47:3 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watasikia mshindo wa kwato za farasi, kelele za magari ya vita, na vishindo vya magurudumu yao. Kina baba watawasahau watoto wao, mikono yao itakuwa imelegea mno.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
kwa sauti ya kwato za farasi wanaoenda mbio, kwa sauti ya magari ya vita ya adui, na mngurumo wa magurudumu yake. Baba hawatageuka kuwasaidia watoto wao, mikono yao italegea.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa sababu ya mshindo wa kukanyaga kwato za farasi wake walio hodari, kwa sababu ya mwendo wa mbiombio wa magari yake ya vita; kwa sababu ya ngurumo ya magurudumu yake, hao akina baba hawatazami nyuma ili kuwaangalia watoto wao, kwa kuwa mikono yao ni dhaifu;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watasikia mshindo wa kwato za farasi, kelele za magari ya vita, na vishindo vya magurudumu yao. Kina baba watawasahau watoto wao, mikono yao itakuwa imelegea mno.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
kwa sauti ya kwato za farasi waendao mbio, kwa sauti ya magari ya adui na mngurumo wa magurudumu yake. Baba hawatageuka kuwasaidia watoto wao, mikono yao italegea.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
kwa sauti ya kwato za farasi waendao mbio, kwa sauti ya magari ya adui na mngurumo wa magurudumu yake. Baba hawatageuka kuwasaidia watoto wao, mikono yao italegea.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa sababu ya kishindo cha kukanyaga kwa kwato za farasi wake walio hodari, kwa sababu ya mwendo wa mbio mbio wa magari yake ya vita; kwa sababu ya mngurumo wa magurudumu yake, hao akina baba hawatazami nyuma ili kuwaangalia watoto wao, kwa kuwa mikono yao ni dhaifu;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watasikia mshindo wa kwato za farasi, kelele za magari ya vita, na vishindo vya magurudumu yao. Kina baba watawasahau watoto wao, mikono yao itakuwa imelegea mno.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa mashindo ya farasi wao wenye nguvu, wakipiga kwato zao, na kwa makelele ya magari yao na kwa uvumi wa magurudumu yao, baba hawatawageukia wana wao, kwani mikono itakuwa imewalegea.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa sababu ya mshindo wa kukanyaga kwato za farasi wake walio hodari, kwa sababu ya mwendo wa mbiombio wa magari yake ya vita; kwa sababu ya ngurumo ya magurudumu yake, hao akina baba hawatazami nyuma ili kuwaangalia watoto wao, kwa kuwa mikono yao ni dhaifu;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watasikia shindo la kwato za farasi, kelele za magari ya vita, na vishindo vya magurudumu yao. Wababa watawasahau watoto wao, mikono yao itakuwa imeregea sana.