Jeremiah 48:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi: “Ole watu wa Nebo, maana mji wake umeharibiwa! Kiriathaimu umeaibishwa, umetekwa, ngome yake imebomolewa mbali;
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kuhusu Moabu: Hili ndilo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu wa Israeli, asemalo: “Ole wake Nebo, kwa maana utaharibiwa. Kiriathaimu utaaibishwa na kutekwa; Misgabu itaaibishwa na kuvunjavunjwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Habari za Moabu. Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Ole wake Nebo! Kwa maana umeharibika; Kiriathaimu umeaibishwa, umetwaliwa; Misgabu umeaibishwa, nao umebomolewa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi: “Ole watu wa Nebo, maana mji wake umeharibiwa! Kiriathaimu umeaibishwa, umetekwa, ngome yake imebomolewa mbali;
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kuhusu Moabu: Hili ndilo BWANA Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: “Ole wa Nebo, kwa maana utaharibiwa. Kiriathaimu utaaibishwa na kutekwa; Misgabu itaaibishwa na kuvunjwa vunjwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kuhusu Moabu: Hili ndilo bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: “Ole wake Nebo, kwa maana utaharibiwa. Kiriathaimu utaaibishwa na kutekwa; Misgabu itaaibishwa na kuvunjavunjwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kuhusu Moabu. BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Ole wake Nebo! Kwa maana umeharibika; Kiriathaimu umeaibishwa, umetwaliwa; Misgabu umeaibishwa, nao umebomolewa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi: “Ole watu wa Nebo, maana mji wake umeharibiwa! Kiriathaimu umeaibishwa, umetekwa, ngome yake imebomolewa mbali;
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yatakayowapata Wamoabu. Hivi ndivyo, Bwana Mwenye vikosi, Mungu wa Isiraeli, anavyosema: Nebo yameupata, kwani umebomolewa! Kiriatemu umepatwa na soni kwa kutekwa, kweli boma lake lililokuwa mlimani limepatwa na soni kwa kustuka.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Habari za Moabu. BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Ole wake Nebo! Kwa maana umeharibika; Kiriathaimu umeaibishwa, umetwaliwa; Misgabu umeaibishwa, nao umebomolewa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Juu ya inchi ya Moabu, Yawe wa majeshi, Mungu wa Israeli, anasema hivi: Ole kwa watu wa Nebo, maana muji wao umeharibiwa! Kiriataimu umepatishwa haya, umetekwa, ukuta wake umebomolewa;