Jeremiah 48:11 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Moabu amestarehe tangu ujana wake, ametulia kama divai katika gudulia. Hajamiminiwa toka chombo hata chombo, hajapata kuchukuliwa uhamishoni. Kwa hiyo yungali na ladha yake, harufu yake nzuri haijabadilika kamwe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Moabu amestarehe tangu ujana wake, kama divai iliyoachwa kwenye machujo yake, haikumiminwa kutoka chombo kimoja hadi kingine, hajaenda uhamishoni. Kwa hiyo ana ladha ile ile kama aliyokuwa nayo, nayo harufu yake haijabadilika.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Moabu amestarehe tangu ujana wake, naye ametulia juu ya sira zake, wala hakumiminwa kutoka chombo kimoja kutiwa chombo kingine, wala hakwenda kufungwa; kwa hiyo ladha yake anakaa nayo, wala harufu yake haikubadilika.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Moabu amestarehe tangu ujana wake, ametulia kama divai katika gudulia. Hajamiminiwa toka chombo hata chombo, hajapata kuchukuliwa uhamishoni. Kwa hiyo yungali na ladha yake, harufu yake nzuri haijabadilika kamwe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Moabu amestarehe tangu ujana wake, kama divai iliyoachwa kwenye machujo yake, haikumiminwa kutoka chombo kimoja hadi kingine, hajaenda uhamishoni. Kwa hiyo ana ladha ile ile kama aliyokuwa nayo, nayo harufu yake haijabadilika.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Moabu amestarehe tangu ujana wake, kama divai iliyoachwa kwenye machujo yake, haikumiminwa kutoka chombo kimoja hadi kingine, hajaenda uhamishoni. Kwa hiyo ana ladha ile ile kama aliyokuwa nayo, nayo harufu yake haijabadilika.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Moabu amestarehe tangu ujana wake, naye ametulia juu ya sira zake, wala hakumiminwa kutoka chombo kimoja kutiwa chombo kingine, wala hakwenda kufungwa; kwa hiyo ladha yake anakaa nayo, wala harufu yake haikubadilika.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Moabu amestarehe tangu ujana wake, ametulia kama divai katika gudulia. Hajamiminiwa toka chombo hata chombo, hajapata kuchukuliwa uhamishoni. Kwa hiyo yungali na ladha yake, harufu yake nzuri haijabadilika kamwe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wamoabu walikaa pasipo kuhangaishwa tangu ujana wao, wakatulia penye mvinyo zao zenye shimbi, hawazitoi chomboni na kumimina katika kingine, wala hawajakwenda kuhamishwa; kwa hiyo yapendezayo vinywa vyao kuyala ni yaleyale, nayo yapendezayo pua zao kuyanusa hayakugeuka.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Moabu amestarehe tangu ujana wake, naye ametulia juu ya sira zake, wala hakumiminwa kutoka chombo kimoja kutiwa chombo kingine, wala hakwenda kufungwa; kwa hiyo ladha yake anakaa nayo, wala harufu yake haikubadilika.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Moabu amestarehe tangu ujana wake, ametulia kama divai katika mutungi. Hajamimiliwa toka chombo kimoja katika chombo kingine, hajapata kupelekwa katika uhamisho. Kwa hiyo angali na onjo yake, harufu yake nzuri haijabadilika hata kidogo.