Jeremiah 48:12 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Kwa hiyo, wakati waja, nasema mimi Mwenyezi-Mungu ambapo nitampelekea wamiminaji ambao wataimimina divai yake. Wataimwaga yote kutoka vyombo vyake na kuvivunja vipandevipande.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini siku zinakuja,” asema Mwenyezi Mungu, “nitakapotuma watu wamiminao kutoka magudulia, nao watamimina; wataacha magudulia yake yakiwa matupu na kuvunja mitungi yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, tazama, siku zinakuja, asema Bwana, ambazo nitampelekea wamiminao, nao watammimina, nao watamwaga vyote vilivyomo vyomboni mwake, na kuzivunja chupa zake vipande vipande.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Kwa hiyo, wakati waja, nasema mimi Mwenyezi-Mungu ambapo nitampelekea wamiminaji ambao wataimimina divai yake. Wataimwaga yote kutoka vyombo vyake na kuvivunja vipandevipande.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini siku zinakuja,” asema BWANA, “nitakapotuma watu wamiminao kutoka kwenye magudulia, nao watammimina; wataacha magudulia yake yakiwa matupu na kuvunja mitungi yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini siku zinakuja,” asema bwana, “nitakapotuma watu wamiminao kutoka kwenye magudulia, nao watamimina; wataacha magudulia yake yakiwa matupu na kuvunja mitungi yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, tazama, siku zinakuja, asema BWANA, ambazo nitatuma kwake wamiminao, nao watammimina, nao watamwaga vyote vilivyomo vyomboni mwake, na kuzivunja chupa zake vipande vipande.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Kwa hiyo, wakati waja, nasema mimi Mwenyezi-Mungu ambapo nitampelekea wamiminaji ambao wataimimina divai yake. Wataimwaga yote kutoka vyombo vyake na kuvivunja vipandevipande.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndivyo, asemavyo Bwana: Kwa hiyo wataona, siku zikija, nitakapotuma kwao mafundi wa mvinyo, watavipindua vyombo vyao na kuzimwaga mvinyo zilizomo, kisha wataivunja hiyo mitungi yao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, tazama, siku zinakuja, asema BWANA, ambazo nitampelekea wamiminao, nao watammimina, nao watamwaga vyote vilivyomo vyomboni mwake, na kuzivunja chupa zake vipande vipande.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hiyo, siku zinakuja ambapo nitamupelekea wamimiaji ambao wataimimia divai yake. –Ni ujumbe wa Yawe.– Wataimwanga yote kutoka vyombo vyake na kuvivunja vipandevipande.