Jeremiah 48:13 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo Wamoabu watamwonea aibu mungu wao Kemoshi, kama vile watu wa Israeli walivyomwonea aibu Betheli, mungu waliyemtegemea.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha Moabu atamwonea aibu Kemoshi, kama vile nyumba ya Israeli walivyoona aibu walipotegemea Betheli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na Moabu ataona haya kwa ajili ya Kemoshi, kama nyumba ya Israeli ilivyoona haya kwa ajili ya Betheli, matumaini yao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo Wamoabu watamwonea aibu mungu wao Kemoshi, kama vile watu wa Israeli walivyomwonea aibu Betheli, mungu waliyemtegemea.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha Moabu atamwonea aibu mungu wao Kemoshi, kama vile nyumba ya Israeli walivyoona aibu wakati walipotegemea mungu wa Betheli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha Moabu atamwonea aibu mungu wao Kemoshi, kama vile nyumba ya Israeli walivyoona aibu walipotegemea mungu wa Betheli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na Moabu ataona haya kwa ajili ya Kemoshi, kama nyumba ya Israeli ilivyoona haya kwa ajili ya Betheli, tegemeo lao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hapo Wamoabu watamwonea aibu mungu wao Kemoshi, kama vile watu wa Israeli walivyomwonea aibu Betheli, mungu waliyemtegemea.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Wamoabu watakapoona soni kwa ajili ya Kemosi, kama walio wa mlango wa Isiraeli walivyoona soni kwa ajili ya Beteli mlimokuwa na egemeo lao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na Moabu ataona haya kwa ajili ya Kemoshi, kama nyumba ya Israeli ilivyoona haya kwa ajili ya Betheli, matumaini yao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu Wamoabu watapata haya kwa ajili ya mungu wao Kemosi, kama vile watu wa Israeli walivyopata haya kwa ajili ya kutegemea Beteli.