Jeremiah 48:15 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwangamizi wa Moabu na miji yake amewasili vijana wake wazuri wamechinjwa. Nimesema mimi mfalme niitwaye Mwenyezi-Mungu wa Majeshi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Moabu ataangamizwa na miji yake itavamiwa, vijana wake wa kiume walio bora sana watachinjwa,” asema Mfalme, ambaye jina lake ni Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Moabu ameharibika, na moshi wa miji yake umepanda; na vijana wake wateule wametelemka kwenda kuchinjwa, asema Mfalme, ambaye jina lake ni Bwana wa majeshi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwangamizi wa Moabu na miji yake amewasili vijana wake wazuri wamechinjwa. Nimesema mimi mfalme niitwaye Mwenyezi-Mungu wa Majeshi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Moabu ataangamizwa na miji yake itavamiwa, vijana wake waume walio bora sana watachinjwa,” asema Mfalme, ambaye jina lake ni BWANA Mungu Mwenye Nguvu Zote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Moabu ataangamizwa na miji yake itavamiwa, vijana wake waume walio bora sana watachinjwa,” asema Mfalme, ambaye jina lake ni bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Moabu ameharibika, na moshi wa miji yake umepanda; na vijana wake wateule wameteremka kwenda kuchinjwa, asema Mfalme, ambaye jina lake ni BWANA wa majeshi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwangamizi wa Moabu na miji yake amewasili vijana wake wazuri wamechinjwa. Nimesema mimi mfalme niitwaye Mwenyezi-Mungu wa Majeshi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wamoabu wataangamia, miji yao itapandiwa, nao vijana wao waliochaguliwa watakuwa hawana budi kutelemka, wauawe; ndivyo, asemavyo Mfalme, Jina lake ni Bwana Mwenye vikosi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Moabu ameharibika, na moshi wa miji yake umepanda; na vijana wake wateule wametelemka kwenda kuchinjwa, asema Mfalme, ambaye jina lake ni BWANA wa majeshi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mwangamizaji wa Moabu na miji yake anashambulia, vijana wake wazuri wamechinjwa. –Ni ujumbe wa Mufalme, jina lake Yawe wa majeshi.–