Jeremiah 48:2 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
fahari ya Moabu imetoweka. Mpango ulifanywa huko Heshboni dhidi yake: ‘Haya! Tuwaangamize wasiwe tena taifa!’ Nawe Madmeni utanyamazishwa, upanga utakufuatia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Moabu haitasifiwa tena; huko Heshboni watu watapanga jinsi ya kumwangusha: ‘Njooni na tuliangamize taifa lile.’ Wewe nawe, ee Madmena, utanyamazishwa; upanga utakufuatia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Sifa za Moabu haziko tena; katika Heshboni wameazimia mabaya juu yake, Haya! Njoni, na tumkatilie mbali asiwe taifa. Wewe nawe, Ee Madmena, utanyamazishwa; upanga utakufuatia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
fahari ya Moabu imetoweka. Mpango ulifanywa huko Heshboni dhidi yake: ‘Haya! Tuwaangamize wasiwe tena taifa!’ Nawe Madmeni utanyamazishwa, upanga utakufuatia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Moabu haitasifiwa tena; huko Heshboni watu watafanya shauri baya la anguko lake: ‘Njoni na tuangamize taifa lile.’ Wewe nawe, Ee Madmeni, utanyamazishwa; upanga utakufuatia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Moabu haitasifiwa tena; huko Heshboni watu watafanya shauri baya la anguko lake: ‘Njooni na tuangamize taifa lile.’ Wewe nawe, ee Madmena, utanyamazishwa; upanga utakufuatia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Sifa za Moabu haziko tena; katika Heshboni wameazimia mabaya juu yake, Haya! Njooni, na tumkatilie mbali asiwe taifa. Wewe nawe, Ee Madmena, utanyamazishwa; upanga utakufuatia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
fahari ya Moabu imetoweka. Mpango ulifanywa huko Heshboni dhidi yake: ‘Haya! Tuwaangamize wasiwe tena taifa!’ Nawe Madmeni utanyamazishwa, upanga utakufuatia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hakuna tena utukufu wa Moabu; mle Hesiboni wanawawazia mabaya kwamba: Twende, tuwang'oe, wasiwe kabila! Nawe Madimeni, utanyamazishwa, panga zitakufuata nyuma.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Sifa za Moabu haziko tena; katika Heshboni wameazimia mabaya juu yake, Haya! Njoni, na tumkatilie mbali asiwe taifa. Wewe nawe, Ee Madmena, utanyamazishwa; upanga utakufuatia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
utukufu wa inchi ya Moabu umetoweka. Mupango ulifanywa huko Hesiboni juu yake: Basi! Tuwaangamize wasikuwe tena taifa! Nawe muji wa Madimeni utanyamazishwa, upanga utakufuatilia.