Jeremiah 48:32 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nakulilia wewe bustani ya Sibma kuliko hata watu wa Yazeri. Matawi yako yametanda mpaka ngambo ya bahari ya Chumvi yakafika hata mpaka Yazeri. Lakini mwangamizi ameyakumba matunda yako ya kiangazi na zabibu zako.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ninalia machozi kwa ajili yenu, kama Yazeri aliavyo, enyi mizabibu ya Sibma. Matawi yako yameenea hadi baharini; yamefika hadi bahari ya Yazeri. Mwangamizi ameyaangukia matunda yako yaliyoiva na mizabibu yako iliyoiva.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nitakulilia, Ee mzabibu wa Sibma, kwa vilio vipitavyo vilio vya Yazeri; matawi yako yalipita juu ya bahari, yalifika hata bahari ya Yazeri; atekaye nyara ameyaangukia matunda yako ya wakati wa jua, na mavuno yako ya zabibu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nakulilia wewe bustani ya Sibma kuliko hata watu wa Yazeri. Matawi yako yametanda mpaka ng'ambo ya bahari ya Chumvi yakafika hata mpaka Yazeri. Lakini mwangamizi ameyakumba matunda yako ya kiangazi na zabibu zako.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ninalia machozi kwa ajili yenu, kama Yazeri aliavyo, Enyi mizabibu ya Sibma. Matawi yako yameenea mpaka baharini; yamefika mpaka Bahari ya Yazeri. Mwarabu ameanguka juu ya matunda yako yaliyoiva na mizabibu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ninalia machozi kwa ajili yenu, kama Yazeri aliavyo, enyi mizabibu ya Sibma. Matawi yako yameenea hadi baharini; yamefika hadi bahari ya Yazeri. Mharabu ameyaangukia matunda yako yaliyoiva na mizabibu yako iliyoiva.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nitakulilia, Ee mzabibu wa Sibma, kwa vilio vipitavyo vilio vya Yazeri; matawi yako yalipita juu ya bahari, yalifika hadi bahari ya Yazeri; atekaye nyara ameyaangukia matunda yako ya wakati wa jua, na mavuno yako ya zabibu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nakulilia wewe bustani ya Sibma kuliko hata watu wa Yazeri. Matawi yako yametanda mpaka ngambo ya bahari ya Chumvi yakafika hata mpaka Yazeri. Lakini mwangamizi ameyakumba matunda yako ya kiangazi na zabibu zako.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kuliko Yazeri ninawalilia ninyi mizabibu ya Sibuma, matawi yenu yaliendelea kufika baharini, yalifika kweli kwenye bahari ya Yazeri; siku za kiangazi walipochuma zabibu zenu, mara mwangamizaji akaja.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nitakulilia, Ee mzabibu wa Sibma, kwa vilio vipitavyo vilio vya Yazeri; matawi yako yalipita juu ya bahari, yalifika hata bahari ya Yazeri; atekaye nyara ameyaangukia matunda yako ya wakati wa jua, na mavuno yako ya zabibu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ninakulilia wewe muzabibu wa Sibuma kuliko hata watu wa Yazeri. Matawi yako yametanda mpaka ngambo ya bahari ya Chumvi, yakafika hata mpaka Yazeri. Lakini mwangamizaji ameyarukia matunda yako ya wakati wa jua na mizabibu yako.