Jeremiah 48:44 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Atakayetoroka kitisho atatumbukia shimoni; atakayetoka shimoni atanaswa mtegoni. Kwa maana nitaleta mambo hayo juu ya Moabu, katika mwaka wao wa adhabu. Nasema mimi Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Yeyote atakayeikimbia hiyo hofu kuu ataanguka ndani ya shimo, yeyote atakayepanda kutoka shimoni, atanaswa katika mtego, kwa sababu nitailetea Moabu mwaka wa adhabu yake,” asema Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Aikimbiaye hofu ataanguka shimoni; na yeye atokaye shimoni atanaswa kwa mtego; maana nitaleta juu yake, yaani, juu ya Moabu, mwaka wa kujiliwa kwake, asema Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Atakayetoroka kitisho atatumbukia shimoni; atakayetoka shimoni atanaswa mtegoni. Kwa maana nitaleta mambo hayo juu ya Moabu, katika mwaka wao wa adhabu. Nasema mimi Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Ye yote atakayeikimbia hiyo hofu kuu ataanguka ndani ya shimo, ye yote atakayepanda kutoka shimoni, atanaswa katika mtego, kwa sababu nitaleta juu ya Moabu mwaka wa adhabu yake,” asema BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Yeyote atakayeikimbia hiyo hofu kuu ataanguka ndani ya shimo, yeyote atakayepanda kutoka shimoni, atanaswa katika mtego, kwa sababu nitaletea Moabu mwaka wa adhabu yake,” asema bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Aikimbiaye hofu ataanguka shimoni; na yeye atokaye shimoni atanaswa kwa mtego; maana nitaleta juu yake, yaani, juu ya Moabu, mwaka wa kujiliwa kwake, asema BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Atakayetoroka kitisho atatumbukia shimoni; atakayetoka shimoni atanaswa mtegoni. Kwa maana nitaleta mambo hayo juu ya Moabu, katika mwaka wao wa adhabu. Nasema mimi Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ayakimbiaye mastuko ataanguka mwinani; atokaye mwinani atakamatwa na tanzi; haya yatakuwa hapo, nitakapowatimilizia hao Wamoabu mwaka wa mapatilizo yao; ndivyo, asemavyo Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Aikimbiaye hofu ataanguka shimoni; na yeye atokaye shimoni atanaswa kwa mtego; maana nitaleta juu yake, yaani, juu ya Moabu, mwaka wa kujiliwa kwake, asema BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Atakayetoroka kitisho atatumbukia ndani ya shimo; atakayetoka ndani ya shimo atanaswa katika mutego. Kwa maana nitaleta mambo hayo juu ya Moabu, katika mwaka wao wa azabu. –Ni ujumbe wa Yawe.