Jeremiah 48:46 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ole wenu watu wa Moabu! Watu wa Kemoshi sasa mmeangamizwa, wana wenu wamechukuliwa mateka, binti zenu wamepelekwa uhamishoni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ole wako, ee Moabu! Watu wa Kemoshi wameangamizwa; watoto wako wa kiume wamepelekwa uhamishoni, na binti zako wamechukuliwa mateka.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ole wako! Ee Moabu, Watu wa Kemoshi wamepotea; Maana wana wako wamechukuliwa mateka, Na binti zako wamekwenda utumwani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ole wenu watu wa Moabu! Watu wa Kemoshi sasa mmeangamizwa, wana wenu wamechukuliwa mateka, binti zenu wamepelekwa uhamishoni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ole wako, Ee Moabu! Watu wa Kemoshi wameangamizwa; wana wako wamepelekwa uhamishoni na binti zako wamechukuliwa mateka.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ole wako, ee Moabu! Watu wa Kemoshi wameangamizwa; wana wako wamepelekwa uhamishoni na binti zako wamechukuliwa mateka.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ole wako! Ee Moabu, Watu wa Kemoshi wamepotea; Maana wana wako wamechukuliwa mateka, Na binti zako wamekwenda utumwani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ole wenu watu wa Moabu! Watu wa Kemoshi sasa mmeangamizwa, wana wenu wamechukuliwa mateka, binti zenu wamepelekwa uhamishoni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yatawapata, ninyi Wamoabu! Ukoo wake Kemosi utaangamia! Kwani wanao wa kiume watachukuliwa kwenda utumwani, nao wanao wa kike watakwenda kuwa vijakazi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ole wako! Ee Moabu, Watu wa Kemoshi wamepotea; Maana wana wako wamechukuliwa mateka, Na binti zako wamekwenda utumwani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ole kwenu watu wa Moabu! Watu wa Kemosi sasa mumeangamizwa, wana wenu wamekamatwa mateka, wabinti zenu wamepelekwa katika utumwa.