Jeremiah 48:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Walionusurika wanapanda kwenda Luhithi huku wanalia kwa sauti. Wanapoteremka kwenda Horonaimu, wanasikia kilio cha uharibifu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wanapanda kwenda njia ya kuelekea Luhithi, wakilia kwa uchungu wanapotembea, kwenye njia inayoshuka kwenda Horonaimu, kilio cha uchungu kwa ajili ya uharibifu kinasikika.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana watu wapandapo huko Luhithi Watapanda wasiache kulia; Nao watu watelemkapo huko Horonaimu Wameisikia huzuni ya kilio cha uharibifu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Walionusurika wanapanda kwenda Luhithi huku wanalia kwa sauti. Wanapoteremka kwenda Horonaimu, wanasikia kilio cha uharibifu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wanapanda kwenda njia ya kuelekea Luhithi, wakilia kwa uchungu wanapotembea, kwenye njia inayoshuka kwenda Horonaimu kilio cha uchungu kwa ajili ya uharibifu kinasikika.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wanapanda kwenda njia ya kuelekea Luhithi, wakilia kwa uchungu wanapotembea, kwenye njia inayoshuka kwenda Horonaimu, kilio cha uchungu kwa ajili ya uharibifu kinasikika.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana watu wapandapo huko Luhithi Watapanda wasiache kulia; Nao watu wateremkapo huko Horonaimu Wameisikia huzuni ya kilio cha uharibifu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Walionusurika wanapanda kwenda Luhithi huku wanalia kwa sauti. Wanapoteremka kwenda Horonaimu, wanasikia kilio cha uharibifu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani njia ya kupandia Luhiti wanaipanda na kulia, hata katika njia ya kutelemkia toka Horonemu kunasikilika yowe zao wasongekao kwa ajili ya mavunjiko kwamba:
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana watu wapandapo huko Luhithi Watapanda wasiache kulia; Nao watu watelemkapo huko Horonaimu Wameisikia huzuni ya kilio cha uharibifu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wale wanaopanda kwenda Luhiti wanalia kwa sauti. Wanapoteremuka kwenda Horonaimu, wanasikia kilio cha uharibifu.