Jeremiah 49:13 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana nimeapa kwa nafsi yangu kwamba mji wa Bosra utakuwa kioja na kichekesho, utakuwa uharibifu na laana; vijiji vyote vitakuwa magofu daima. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ninaapa kwa nafsi yangu,” asema Mwenyezi Mungu, “kwamba Bosra utakuwa magofu na kitu cha kutisha, cha aibu na cha kulaania; miji yake yote itakuwa magofu milele.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana nimeapa kwa nafsi yangu, asema Bwana, kwamba Bozra utakuwa ajabu, na aibu, na ukiwa, na laana; na miji yake yote itakuwa ukiwa wa daima.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana nimeapa kwa nafsi yangu kwamba mji wa Bosra utakuwa kioja na kichekesho, utakuwa uharibifu na laana; vijiji vyote vitakuwa magofu daima. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ninaapa kwa nafsi yangu,” asema BWANA, “kwamba Bosra utakuwa magofu na kitu cha kutisha, cha aibu na cha kulaania; miji yake yote itakuwa magofu milele.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ninaapa kwa nafsi yangu,” asema bwana, “kwamba Bosra utakuwa magofu na kitu cha kutisha, cha aibu na cha kulaania; miji yake yote itakuwa magofu milele.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana nimeapa kwa nafsi yangu, asema BWANA, kwamba Bozra utakuwa ajabu, na aibu, na ukiwa, na laana; na miji yake yote itakuwa ukiwa wa daima.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana nimeapa kwa nafsi yangu kwamba mji wa Bosra utakuwa kioja na kichekesho, utakuwa uharibifu na laana; vijiji vyote vitakuwa magofu daima. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndivyo, asemavyo Bwana: Nimejiapia mwenyewe kwamba: Bosira sharti ustukiwe kwa kutiwa soni, ukae peke yake kwa kuapizwa, nayo miji yake yote itakuwa mabomoko kale na kale.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana nimeapa kwa nafsi yangu, asema BWANA, kwamba Bozra utakuwa ajabu, na aibu, na ukiwa, na laana; na miji yake yote itakuwa ukiwa wa daima.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Maana nimeapa kwa nafsi yangu kwamba muji wa Bosira utakuwa kitisho na mushangao, utakuwa uharibifu na kutumiwa kama mufano wa laana; vijiji vyote vitakuwa mabomoko siku zote. –Ni ujumbe wa Yawe.