Jeremiah 49:16 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Vitisho unavyotoa na kiburi chako vimekudanganya, ewe ukaaye katika mapango ya miamba, unayeishi juu ya kilele cha mlima! Ingawa unaweka makao yako juu kama ya tai, mimi nitakuporomosha kutoka huko uliko. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Vitisho vyako na kiburi cha moyo wako vimekudanganya, wewe unayeishi katika majabali ya miamba, wewe unayedumu katika miinuko ya kilima. Ujapojenga kiota chako juu sana kama cha tai, nitakushusha chini kutoka huko,” asema Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Katika habari za kuogofya kwako, Kiburi cha moyo wako kimekudanganya, Wewe ukaaye katika pango za majabali, Ushikaye kilele cha milima; Ujapofanya kioto chako juu sana kama tai, Nitakushusha kutoka huko; asema Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Vitisho unavyotoa na kiburi chako vimekudanganya, ewe ukaaye katika mapango ya miamba, unayeishi juu ya kilele cha mlima! Ingawa unaweka makao yako juu kama ya tai, mimi nitakuporomosha kutoka huko uliko. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Vitisho vyako na kiburi cha moyo wako vimekudanganya, wewe unayeishi katika majabali ya miamba, wewe unayemiliki katika miinuko ya kilima. Ujapojenga kiota chako juu sana kama cha tai, kutoka huko nitakushusha chini,” asema BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Vitisho vyako na kiburi cha moyo wako vimekudanganya, wewe unayeishi katika majabali ya miamba, wewe unayedumu katika miinuko ya kilima. Ujapojenga kiota chako juu sana kama cha tai, nitakushusha chini kutoka huko,” asema bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kuhusu kuogofya kwako, Kiburi cha moyo wako kimekudanganya, Wewe ukaaye katika pango za majabali, Ushikaye kilele cha milima; Ujapofanya kiota chako juu sana kama tai, Nitakushusha kutoka huko; asema BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Vitisho unavyotoa na kiburi chako vimekudanganya, ewe ukaaye katika mapango ya miamba, unayeishi juu ya kilele cha mlima! Ingawa unaweka makao yako juu kama ya tai, mimi nitakuporomosha kutoka huko uliko. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kuogopesha kwenu ni majivuno tu ya mioyo yenu yaliyowadanganya, kwa kuwa mnakaa nyufani kwenye miamba, mkagandamana na milima mirefu. Lakini ijapo mvijenge vituo vyenu juu kabisa kama tai, huko nako nitawashusha; ndivyo, asemavyo Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Katika habari za kuogofya kwako, Kiburi cha moyo wako kimekudanganya, Wewe ukaaye katika pango za majabali, Ushikaye kilele cha milima; Ujapofanya kioto chako juu sana kama tai, Nitakushusha kutoka huko; asema BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Vitisho unavyotoa na kiburi chako vimekudanganya, ewe unayekaa katika mapango ya mawe, unayeishi juu ya kilele cha mulima! Ingawa unaweka makao yako juu kama ya tai, mimi nitakuporomosha kutoka huko unakokuwa. –Ni ujumbe wa Yawe.