Jeremiah 49:22 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tazama, adui atapanda juu na kuruka kama tai na kutandaza mabawa yake juu ya Bosra. Siku hiyo moyo wa mashujaa wa Edomu utakumbwa na hofu kama ya mwanamke anayejifungua.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Tazama! Tai atapaa juu angani na kuruka chini kwa ghafula, akitandaza mabawa yake juu ya Bosra. Katika siku hiyo, mioyo ya mashujaa wa Edomu itakuwa kama moyo wa mwanamke katika uchungu wa kuzaa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tazama, atapanda na kuruka kama tai, na kutandaza mabawa yake juu ya Bozra; na mioyo ya mashujaa wa Edomu siku hiyo itakuwa kama moyo wa mwanamke katika utungu wake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tazama, adui atapanda juu na kuruka kama tai na kutandaza mabawa yake juu ya Bosra. Siku hiyo moyo wa mashujaa wa Edomu utakumbwa na hofu kama ya mwanamke anayejifungua.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Tazama! Tai atapaa juu angani na kuruka chini kwa ghafula, akitandaza mbawa zake juu ya Bosra. Katika siku hiyo, mioyo ya mashujaa wa Edomu itakuwa kama moyo wa mwanamke aliye katika utungu wa kuzaa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Tazama! Tai atapaa juu angani na kuruka chini kwa ghafula, akitandaza mabawa yake juu ya Bosra. Katika siku hiyo, mioyo ya mashujaa wa Edomu itakuwa kama moyo wa mwanamke katika utungu wa kuzaa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tazama, atapanda na kuruka kama tai, na kutandaza mabawa yake juu ya Bozra; na mioyo ya mashujaa wa Edomu siku hiyo itakuwa kama moyo wa mwanamke akiwa katika uchungu wa kujifungua.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tazama, adui atapanda juu na kuruka kama tai na kutandaza mabawa yake juu ya Bosra. Siku hiyo moyo wa mashujaa wa Edomu utakumbwa na hofu kama ya mwanamke anayejifungua.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tazameni, anaurukia Bosira kama kozi na kuukunjulia mabawa yake. Kwa hiyo mioyo ya wapiga vita wa Edomu itakuwa siku ile kama moyo wa mwanamke anayetaka kuzaa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tazama, atapanda na kuruka kama tai, na kutandaza mabawa yake juu ya Bozra; na mioyo ya mashujaa wa Edomu siku hiyo itakuwa kama moyo wa mwanamke katika utungu wake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Adui atapanda juu na kuruka kama tai na kutandaza mabawa yake juu ya Bosira. Siku hiyo moyo wa mashujaa wa Edomu utakuwa kama vile moyo wa mwanamuke anayezaa.