Jeremiah 49:24 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu wa Damasko wamekufa moyo; wamegeuka wapate kukimbia; hofu kubwa imewakumba, uchungu na huzuni vimewapata, kama mwanamke anayejifungua
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Dameski amedhoofika, amegeuka na kukimbia, hofu ya ghafula imemkamata sana; amepatwa na uchungu na maumivu, maumivu kama ya mwanamke katika uchungu wa kuzaa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Dameski umedhoofika; Umejigeuza kukimbia; tetemko limeushika; Dhiki na huzuni zimeupata, Kama za mwanamke katika utungu wake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu wa Damasko wamekufa moyo; wamegeuka wapate kukimbia; hofu kubwa imewakumba, uchungu na huzuni vimewapata, kama mwanamke anayejifungua
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Dameski amedhoofika, amegeuka na kukimbia, hofu ya ghafula imemkamata sana; amepatwa na uchungu na maumivu, maumivu kama ya mwanamke aliye katika utungu wa kuzaa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Dameski amedhoofika, amegeuka na kukimbia, hofu ya ghafula imemkamata sana; amepatwa na uchungu na maumivu, maumivu kama ya mwanamke katika utungu wa kuzaa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Dameski umedhoofika; Umejigeuza kukimbia; tetemeko limeushika; Dhiki na huzuni zimeupata, Kama za mwanamke katika uchungu wake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu wa Damasko wamekufa moyo; wamegeuka wapate kukimbia; hofu kubwa imewakumba, uchungu na huzuni vimewapata, kama mwanamke anayejifungua
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wadamasko wamelegea, wakageuka, wakimbie, mtetemeko ukawashika, masongano na machungu yakawapata kama mwanamke anayetaka kuzaa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Dameski umedhoofika; Umejigeuza kukimbia; tetemko limeushika; Dhiki na huzuni zimeupata, Kama za mwanamke katika utungu wake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu wa Damasiki wamevunjika moyo; wamegeuka kusudi wapate kukimbia; hofu kubwa imewashika, uchungu na huzuni vimewapata, kama mwanamuke anayezaa.