Jeremiah 49:28 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kuhusu Kedari na falme za Hazori ambazo Nebukadneza mfalme wa Babuloni, alizishambulia na kuzishinda, Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Inuka uende kulishambulia kabila la Kedari! Waangamize watu wa mashariki!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kuhusu Kedari na falme za Hazori, ambazo Nebukadneza mfalme wa Babeli alizishambulia: Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: “Inuka, ushambulie Kedari na kuwaangamiza watu wa mashariki.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Habari za Kedari, na za falme za Hazori, ambazo Nebukadreza, mfalme wa Babeli, alizipiga. Bwana asema hivi, Ondokeni, pandeni hata Kedari, mkawateke nyara wana wa mashariki.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kuhusu Kedari na falme za Hazori ambazo Nebukadneza mfalme wa Babuloni, alizishambulia na kuzishinda, Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Inuka uende kulishambulia kabila la Kedari! Waangamize watu wa mashariki!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kuhusu Kedari na falme za Hazori, ambazo Nebukadneza mfalme wa Babeli alizishambulia: Hili ndilo asemalo BWANA: “Inuka, ushambulie Kedari na kuwaangamiza watu wa mashariki.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kuhusu Kedari na falme za Hazori, ambazo Nebukadneza mfalme wa Babeli alizishambulia: Hili ndilo asemalo bwana: “Inuka, ushambulie Kedari na kuwaangamiza watu wa mashariki.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kuhusu Kedari, na falme za Hazori, ambazo Nebukadneza, mfalme wa Babeli, alizipiga. BWANA asema hivi, Ondokeni, pandeni hadi Kedari, mkawateke nyara wana wa mashariki.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kuhusu Kedari na falme za Hazori ambazo Nebukadneza mfalme wa Babuloni, alizishambulia na kuzishinda, Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Inuka uende kulishambulia kabila la Kedari! Waangamize watu wa mashariki!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yatakayoipata nchi ya Kedari nazo nchi za kifalme za Hasori, Nebukadinesari, mfalme wa Babeli, alizozipiga. Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Inukeni, mpande kwenda Kedari, mwaangamize wana wa nchi iliyoko maawioni kwa jua!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Habari za Kedari, na za falme za Hazori, ambazo Nebukadreza, mfalme wa Babeli, alizipiga. BWANA asema hivi, Ondokeni, pandeni hata Kedari, mkawateke nyara wana wa mashariki.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Juu ya Kedari na falme za Hazori ambazo Nebukadneza mufalme wa Babeli alizishambulia na kuzishinda, Yawe anasema hivi: Simama uende kulishambulia kabila la Kedari! Uwaangamize watu wa mashariki!