Jeremiah 49:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Ombolezeni, enyi watu wa Heshboni, maana mji wa Ai umeharibiwa! Lieni enyi binti za Raba! Jifungeni mavazi ya gunia viunoni ombolezeni na kukimbia huko na huko uani! Maana mungu Milkomu atapelekwa uhamishoni, pamoja na makuhani wake na watumishi wake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Lia kwa huzuni, ee Heshboni, kwa kuwa Ai umeangamizwa! Pigeni kelele, enyi wakazi wa Raba! Vaeni gunia na kuomboleza, kimbieni hapa na pale ndani ya kuta, kwa kuwa Moleki ataenda uhamishoni, yeye pamoja na makuhani na maafisa wake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Piga yowe, Ee Heshboni, Kwa maana Ai umeangamizwa; Lieni, enyi binti za Raba, Mjivike nguo za magunia; Ombolezeni, mkipiga mbio Huko na huko kati ya maboma; Maana Malkamu atakwenda kuhamishwa, Makuhani wake na wakuu wake pamoja.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Ombolezeni, enyi watu wa Heshboni, maana mji wa Ai umeharibiwa! Lieni enyi binti za Raba! Jifungeni mavazi ya gunia viunoni ombolezeni na kukimbia huko na huko uani! Maana mungu Milkomu atapelekwa uhamishoni, pamoja na makuhani wake na watumishi wake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Lia kwa huzuni, Ee Heshboni, kwa kuwa Ai umeangamizwa! Piga kelele, Enyi wakazi wa Raba! Vaeni nguo ya gunia na kuomboleza, kimbieni hapa na pale ndani ya kuta, kwa kuwa Moleki atakwenda uhamishoni, yeye pamoja na makuhani na maafisa wake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Lia kwa huzuni, ee Heshboni, kwa kuwa Ai umeangamizwa! Pigeni kelele, enyi wakazi wa Raba! Vaeni nguo za gunia na kuomboleza, kimbieni hapa na pale ndani ya kuta, kwa kuwa Moleki atakwenda uhamishoni, yeye pamoja na makuhani na maafisa wake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Omboleza, Ee Heshboni, Kwa maana Ai umeangamizwa; Lieni, enyi binti za Raba, Mjivike nguo za magunia; Ombolezeni, mkipiga mbio Huko na huko kati ya maboma; Maana Malkamu atakwenda kuhamishwa, Makuhani wake na wakuu wake pamoja.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Ombolezeni, enyi watu wa Heshboni, maana mji wa Ai umeharibiwa! Lieni enyi binti za Raba! Jifungeni mavazi ya gunia viunoni ombolezeni na kukimbia huko na huko uani! Maana mungu Milkomu atapelekwa uhamishoni, pamoja na makuhani wake na watumishi wake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Pigeni vilio, ninyi wa Hesiboni, ya kuwa Ai umebomolewa! Pigeni makelele, ninyi wanawali wa Raba! Jifungeni magunia! Ombolezeni na kwenda huko na huko penye nyua! Kwani Malkamu atakwenda kutekwa na kuhamishwa pamoja na watambikaji wake na wakuu wake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Piga yowe, Ee Heshboni, Kwa maana Ai umeangamizwa; Lieni, enyi binti za Raba, Mjivike nguo za magunia; Ombolezeni, mkipiga mbio Huko na huko kati ya maboma; Maana Malkamu atakwenda kuhamishwa, Makuhani wake na wakuu wake pamoja.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Muomboleze, enyi watu wa Hesiboni, maana muji Ai umeharibika! Mulie, enyi wabinti wa Raba! Muvae magunia, muomboleze na kukimbia huko na huko ndani ya ukuta wenu! Maana mungu Milkomu atapelekwa katika uhamisho, pamoja na makuhani wake na watumishi wake.