Jeremiah 49:30 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kimbieni, nendeni mbali, kaeni mashimoni. Enyi wakazi wa Haziri, kimbieni mtangetange na kukaa mafichoni! Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema. Maana Nebukadneza mfalme wa Babuloni, amefanya mpango dhidi yenu, amepania kuja kuwashambulia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Kimbieni haraka! Kaeni kwenye mapango marefu sana, ninyi mnaoishi Hazori,” asema Mwenyezi Mungu. “Nebukadneza, mfalme wa Babeli amepanga njama dhidi yenu; amebuni hila dhidi yenu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kimbieni ninyi, enendeni mbali mkitanga-tanga, kaeni chini sana, enyi mkaao Hazori, asema Bwana; maana Nebukadreza, mfalme wa Babeli, amefanya shauri juu yenu, naye amekusudia neno juu yenu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kimbieni, nendeni mbali, kaeni mashimoni. Enyi wakazi wa Haziri, kimbieni mtangetange na kukaa mafichoni! Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema. Maana Nebukadneza mfalme wa Babuloni, amefanya mpango dhidi yenu, amepania kuja kuwashambulia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Kimbieni haraka! Kaeni kwenye mapango marefu sana, ninyi mkaao Hazori,” asema BWANA. “Nebukadneza, mfalme wa Babeli amepanga shauri baya dhidi yenu; amebuni hila dhidi yenu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Kimbieni haraka! Kaeni kwenye mapango marefu sana, ninyi mkaao Hazori,” asema bwana. “Nebukadneza, mfalme wa Babeli amepanga shauri baya dhidi yenu; amebuni hila dhidi yenu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kimbieni ninyi, nendeni mbali mkitangatanga, kaeni chini sana, enyi mkaao Hazori, asema BWANA; maana Nebukadneza, mfalme wa Babeli, amefanya shauri juu yenu, naye amekusudia neno juu yenu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kimbieni, nendeni mbali, kaeni mashimoni. Enyi wakazi wa Haziri, kimbieni mtangetange na kukaa mafichoni! Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema. Maana Nebukadneza mfalme wa Babuloni, amefanya mpango dhidi yenu, amepania kuja kuwashambulia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kimbieni na kupiga mbio sana! Chimbeni mashimo ya kukaa ndani yao, ninyi mkaao Hasori! ndivyo, asemavyo Bwana; kwani Nebukadinesari, mfalme wa Babeli, amewakatia shauri na kuwawazia mawazo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kimbieni ninyi, enendeni mbali mkitanga-tanga, kaeni chini sana, enyi mkaao Hazori, asema BWANA; maana Nebukadreza, mfalme wa Babeli, amefanya shauri juu yenu, naye amekusudia neno juu yenu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mukimbie, muende mbali, mukae ndani ya mashimo. Enyi wakaaji wa Hazori, mukimbie, mutangetange na kujificha mbali! –Ni ujumbe wa Yawe.– Maana Nebukadneza mufalme wa Babeli, amefanya mupango juu yenu, amekusudia kuja kuwashambulia.