Jeremiah 49:32 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Ngamia wao watatekwa mifugo yao itachukuliwa mateka. Nitawatawanya kila upande, watu wale wanaonyoa denge. Nitawaletea maafa kutoka kila upande. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ngamia wao watakuwa nyara, nayo mifugo yao itatekwa. Walio maeneo ya mbali nitawatawanya pande zote, nami nitaleta maafa juu yao kutoka kila upande,” asema Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na ngamia zao watakuwa mateka, na wingi wa makundi yao utakuwa nyara; nami nitawatawanya hata pepo zote watu wale wanyoao denge; nami nitaleta msiba wao toka pande zao zote, asema Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Ngamia wao watatekwa mifugo yao itachukuliwa mateka. Nitawatawanya kila upande, watu wale wanaonyoa denge. Nitawaletea maafa kutoka kila upande. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ngamia wao watakuwa nyara, nayo makundi yao makubwa ya ng'ombe yatatekwa. Wale walio maeneo ya mbali nitawatawanya pande zote nami nitaleta maafa juu yao kutoka kila upande,” asema BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ngamia wao watakuwa nyara, nayo makundi yao makubwa ya ng’ombe yatatekwa. Wale walio maeneo ya mbali nitawatawanya pande zote, nami nitaleta maafa juu yao kutoka kila upande,” asema bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na ngamia wao watakuwa mateka, na wingi wa makundi yao utakuwa nyara; nami nitawatawanya pande zote watu wale wanyoao denge; nami nitaleta msiba wao toka pande zao zote, asema BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Ngamia wao watatekwa mifugo yao itachukuliwa mateka. Nitawatawanya kila upande, watu wale wanaonyoa denge. Nitawaletea maafa kutoka kila upande. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ngamia wao watakuwa mateka yenu, nao kondoo na mbuzi wao wengi mno watakuwa mapato yenu. Wao wenyewe wanyoao denge nitawatawanya kwenda pande zote, upepo utokako, nikiwaletea maangamizo, yawatokee po pote; ndivyo, asemavyo Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na ngamia zao watakuwa mateka, na wingi wa makundi yao utakuwa nyara; nami nitawatawanya hata pepo zote watu wale wanyoao denge; nami nitaleta msiba wao toka pande zao zote, asema BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ngamia wao watatekwa, makundi yao ya nyama yatanyanganywa. Nitawasambaza kila upande, watu wale wanaonyoa nywele zote za pembenipembeni ya kichwa. Nitawaletea hasara kutoka kila upande. –Ni ujumbe wa Yawe.