Jeremiah 49:37 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nitawafadhaisha watu wa Elamu mbele ya maadui zao na mbele ya wale wanaotaka kuyaangamiza maisha yao. Nitawaletea maafa na hasira yangu kali. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema. Nitawaletea upanga kuwafuata mpaka niwaangamize kabisa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nitamfadhaisha Elamu mbele ya adui zao, mbele yao wanaoutafuta uhai wao; nitaleta maafa juu yao, naam, hasira yangu kali,” asema Mwenyezi Mungu. “Nitawafuatia kwa upanga hadi nitakapowamaliza.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nami nitawafadhaisha watu wa Elamu mbele ya adui zao, na mbele ya hao wanaowatafuta roho zao; nami nitawaletea mabaya, naam, hasira yangu kali, asema Bwana; nami nitautuma upanga uwafuatie, hata nitakapowaangamiza;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nitawafadhaisha watu wa Elamu mbele ya maadui zao na mbele ya wale wanaotaka kuyaangamiza maisha yao. Nitawaletea maafa na hasira yangu kali. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema. Nitawaletea upanga kuwafuata mpaka niwaangamize kabisa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nitamfadhaisha Elamu mbele ya adui zao, mbele yao wale wanaotafuta uhai wao; nitaleta maafa juu yao, pia hasira yangu kali,” asema BWANA. “Nitawafuatia kwa upanga mpaka nitakapowamaliza.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nitamfadhaisha Elamu mbele ya adui zao, mbele yao wale wanaotafuta uhai wao; nitaleta maafa juu yao, naam, hasira yangu kali,” asema bwana. “Nitawafuatia kwa upanga mpaka nitakapowamaliza.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nami nitawafadhaisha watu wa Elamu mbele ya adui zao, na mbele ya hao wanaowatafuta roho zao; nami nitawaletea mabaya, naam, hasira yangu kali, asema BWANA; nami nitautuma upanga uwafuatie, hadi nitakapowaangamiza;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nitawafadhaisha watu wa Elamu mbele ya maadui zao na mbele ya wale wanaotaka kuyaangamiza maisha yao. Nitawaletea maafa na hasira yangu kali. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema. Nitawaletea upanga kuwafuata mpaka niwaangamize kabisa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nitawastusha Waelamu, wawaogope adui zao nao wazitafutao roho zao; kisha nitawaletea mabaya, makali yangu yenye moto yatakapowawakia, mpaka niwamalize.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nami nitawafadhaisha watu wa Elamu mbele ya adui zao, na mbele ya hao wanaowatafuta roho zao; nami nitawaletea mabaya, naam, hasira yangu kali, asema BWANA; nami nitautuma upanga uwafuatie, hata nitakapowaangamiza;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nitawafazaisha watu wa Elamu mbele ya waadui zao na mbele ya wale wanaotaka kuyaangamiza maisha yao. Nitawaletea hasara na hasira yangu kali. –Ni ujumbe wa Yawe.– Nitawashambulia kwa upanga mpaka niwaangamize kabisa.