Jeremiah 49:4 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mbona mnajivunia mabonde yenu, enyi msioamini, watu mliotegemea mali zenu, mkisema: ‘Nani atathubutu kupigana nasi?’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa nini unajivunia mabonde yako, kujivunia mabonde yako yaliyozaa sana? Ee binti usiye mwaminifu, unayeutumainia utajiri wako na kusema, ‘Ni nani atakayenishambulia?’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mbona unajisifu kwa sababu ya mabonde, bonde lako litiririkalo, Ee binti mwenye kuasi? Utumainiaye hazina zako, ukisema, Ni nani atakayenijilia?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mbona mnajivunia mabonde yenu, enyi msioamini, watu mliotegemea mali zenu, mkisema: ‘Nani atathubutu kupigana nasi?’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa nini unajivunia mabonde yako, ukijivunia mabonde yako yaliyozaa sana? Ee binti usiye mwaminifu, unayeutumainia utajiri wako na kusema, ‘Ni nani atakayenishambulia?’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa nini unajivunia mabonde yako, kujivunia mabonde yako yaliyozaa sana? Ee binti usiye mwaminifu, unayeutumainia utajiri wako na kusema, ‘Ni nani atakayenishambulia?’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mbona unajisifu kwa sababu ya mabonde, bonde lako litiririkalo, Ee binti mwenye kuasi? Utumainiaye hazina zako, ukisema, Ni nani atakayenijia?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mbona mnajivunia mabonde yenu, enyi msioamini, watu mliotegemea mali zenu, mkisema: ‘Nani atathubutu kupigana nasi?’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mnayasifiaje mabonde zaidi, mlio na bonde lichuruzikalo maji, ninyi wanawali wakatavu? Mnaviegemea vilimbiko vyenu kwamba: Yuko nani atakayenijia?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mbona unajisifu kwa sababu ya mabonde, bonde lako litiririkalo, Ee binti mwenye kuasi? Utumainiaye hazina zako, ukisema, Ni nani atakayenijilia?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mbona munajivunia mabonde yenu, enyi musiokuwa waaminifu, ninyi watu muliotegemea mali zenu, mukisema: Nani atasubutu kupigana nasi?