Jeremiah 49:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wachuma zabibu watakapokuja kwenu hawatabakiza hata zabibu moja. Usiku ule wezi watakapofika, wataharibu kila kitu mpaka watosheke.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Je, kama wachuma zabibu wangekuja kwako, wasingebakiza zabibu chache? Kama wezi wangekujia usiku, je, si wangeiba tu kiasi ambacho wangehitaji?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Je! Kama wachuma zabibu wangekujia, wasingeacha zabibu ziokotwe? Kama wangekujia wevi usiku, wasingeharibu hata watakapopata vya kutosha?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wachuma zabibu watakapokuja kwenu hawatabakiza hata zabibu moja. Usiku ule wezi watakapofika, wataharibu kila kitu mpaka watosheke.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Je, kama wachuma zabibu wangekuja kwako, wasingebakiza zabibu chache? Kama wezi wangekuja usiku, je, si wangeiba kiasi ambacho wangehitaji tu?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Je, kama wachuma zabibu wangekuja kwako, wasingebakiza zabibu chache? Kama wezi wangekujia usiku, je, si wangeiba tu kiasi ambacho wangehitaji?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Je! Kama wachuma zabibu wangekujia, wasingeacha zabibu ziokotwe? Kama wangekujia wezi usiku, wasingeharibu hata watakapopata vya kutosha?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wachuma zabibu watakapokuja kwenu hawatabakiza hata zabibu moja. Usiku ule wezi watakapofika, wataharibu kila kitu mpaka watosheke.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kama wachuma zabibu wanakujia, hawasazi za kuokoteza; kama wezi wanakujia na usiku, hupokonya, mpaka wakitoshewa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Je! Kama wachuma zabibu wangekujia, wasingeacha zabibu ziokotwe? Kama wangekujia wevi usiku, wasingeharibu hata watakapopata vya kutosha?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wachuma zabibu watakapokuja kwenu, hawataacha hata zabibu moja. Usiku ule wizi watakapofika, wataharibu kila kitu mpaka watosheke.