Jeremiah 5:1 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kimbieni huko na huko mjini Yerusalemu; pelelezeni na kujionea wenyewe! Chunguzeni masoko yake mwone kama kuna mtu atendaye haki mtu atafutaye ukweli; akiwako, basi Mwenyezi-Mungu atausamehe Yerusalemu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Pandeni na kushuka katika mitaa ya Yerusalemu, tazameni pande zote na mtafakari, tafuteni katika viwanja vyake. Kama mtaweza kumpata hata mtu mmoja tu atendaye kwa uaminifu na kutafuta kweli, nitausamehe mji huu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Pigeni mbio huku na huku katika njia za Yerusalemu, mkaone sasa, na kujua, na kutafuta katika viwanja vyake, kwamba mwaweza kumpata mtu mmoja, kwamba yuko mtu mmoja awaye yote atendaye kwa haki, atafutaye uaminifu; nami nitausamehe mji huo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kimbieni huko na huko mjini Yerusalemu; pelelezeni na kujionea wenyewe! Chunguzeni masoko yake mwone kama kuna mtu atendaye haki mtu atafutaye ukweli; akiwako, basi Mwenyezi-Mungu atausamehe Yerusalemu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Pandeni na kushuka katika mitaa ya Yerusalemu, tazameni pande zote na mkumbuke, tafuteni katika viwanja vyake. Kama mtaweza kumpata hata mtu mmoja tu atendaye kwa uaminifu na kutafuta kweli, nitausamehe mji huu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Pandeni na kushuka katika mitaa ya Yerusalemu, tazameni pande zote na mtafakari, tafuteni katika viwanja vyake. Kama mtaweza kumpata hata mtu mmoja tu atendaye kwa uaminifu na kutafuta kweli, nitausamehe mji huu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Pigeni mbio huku na huku katika njia za Yerusalemu, mkaone sasa, na kujua, na kutafuta katika viwanja vyake, kwamba mwaweza kumpata mtu mmoja, kwamba yuko mtu mmoja awaye yote atendaye kwa haki, atafutaye uaminifu; nami nitausamehe mji huo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kimbieni huko na huko mjini Yerusalemu; pelelezeni na kujionea wenyewe! Chunguzeni masoko yake mwone kama kuna mtu atendaye haki mtu atafutaye ukweli; akiwako, basi Mwenyezi-Mungu atausamehe Yerusalemu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tembeeni katika barabara za Yerusalemu! Tazameni, mjue! Tafuteni katika viwanja vyake, kama mnaona mtu awaye yote afanyaye yanyokayo, atafutaye welekevu! Ndipo, nitakapowaondolea makosa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Pigeni mbio huku na huku katika njia za Yerusalemu, mkaone sasa, na kujua, na kutafuta katika viwanja vyake, kwamba mwaweza kumpata mtu mmoja, kwamba yuko mtu mmoja awaye yote atendaye kwa haki, atafutaye uaminifu; nami nitausamehe mji huo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mukimbie huko na huko katika Yerusalema, mupeleleze na kujionea wenyewe, muchunguze katika masoko yake. Mukiona hata mutu mumoja anayefuata sheria, mutu anayetafuta ukweli, basi Yawe atausamehe Yerusalema.