Jeremiah 5:15 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Nami Mwenyezi-Mungu nasema juu yenu enyi Waisraeli: Mimi naleta taifa moja kutoka mbali, lije kuwashambulia. Taifa ambalo halishindiki, taifa ambalo ni la zamani, ambalo lugha yake hamuifahamu, wala hamwezi kuelewa wasemacho.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ee nyumba ya Israeli,” asema Mwenyezi Mungu, “Ninaleta taifa toka mbali dhidi yako, taifa la kale na linaloendelea kudumu, taifa ambalo lugha yao huijui, wala msemo wao huwezi kuuelewa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Angalia, nitaleta taifa juu yenu litokalo mbali sana, Ee nyumba ya Israeli, asema Bwana; ni taifa hodari, ni taifa la zamani sana, taifa ambalo hujui lugha yake, wala huyafahamu wasemayo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Nami Mwenyezi-Mungu nasema juu yenu enyi Waisraeli: Mimi naleta taifa moja kutoka mbali, lije kuwashambulia. Taifa ambalo halishindiki, taifa ambalo ni la zamani, ambalo lugha yake hamuifahamu, wala hamwezi kuelewa wasemacho.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ee nyumba ya Israeli,” asema BWANA, “Ninaleta taifa toka mbali dhidi yako, taifa la kale na linaloendelea kudumu, taifa ambalo lugha yao huijui, wala msemo wao huwezi kuuelewa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ee nyumba ya Israeli,” asema bwana, “Ninaleta taifa toka mbali dhidi yako, taifa la kale na linaloendelea kudumu, taifa ambalo lugha yao huijui, wala msemo wao huwezi kuuelewa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Angalia, nitaleta taifa juu yenu litokalo mbali sana, Ee nyumba ya Israeli, asema BWANA; ni taifa hodari, ni taifa la zamani sana, taifa ambalo hujui lugha yake, wala huyafahamu wasemayo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Nami Mwenyezi-Mungu nasema juu yenu enyi Waisraeli: Mimi naleta taifa moja kutoka mbali, lije kuwashambulia. Taifa ambalo halishindiki, taifa ambalo ni la zamani, ambalo lugha yake hamuifahamu, wala hamwezi kuelewa wasemacho.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mtaniona, ninyi wa mlango wa Isiraeli, nikiwaletea taifa litokalo mbali, ndio watu wenye nguvu, ndio watu wa kale, ndio watu, usiowajua msemo wao, usiwasikie, wakisema; ndivyo, asemavyo Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Angalia, nitaleta taifa juu yenu litokalo mbali sana, Ee nyumba ya Israeli, asema BWANA; ni taifa hodari, ni taifa la zamani sana, taifa ambalo hujui lugha yake, wala huyafahamu wasemayo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na kwa ngambo yenu ninyi watu wa Israeli, ninaleta taifa moja kutoka mbali kuwashambulia. –Ni ujumbe wa Yawe.– Hili taifa haliwezi kushindwa, ni taifa la zamani, ni taifa ambalo hamufahamu luga yake. Hamuwezi kuelewa hata neno wanalolisema.