Jeremiah 5:17 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watayala mazao yenu na chakula chenu; watawamaliza watoto wenu wa kike na wa kiume. Watachinja makundi yenu ya kondoo na ng'ombe; wataiharibu mizabibu yenu na mitini yenu. Miji yenu ya ngome mnayoitegemea, wataiharibu kwa silaha zao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Watayaangamiza mazao yenu na chakula chenu, watawaangamiza wana wenu wa kiume na wa kike; watayaangamiza makundi yenu ya kondoo na ya ng’ombe, wataiangamiza mizabibu yenu na mitini yenu. Kwa upanga wataiangamiza miji yenye ngome mliyoitumainia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao watakula mavuno yako, na mkate wako, ambao iliwapasa wana wako na binti zako kuula; watakula makundi yako ya kondoo na ya ng'ombe; watakula mizabibu yako na mitini yako; wataiharibu miji yako yenye boma, uliyokuwa ukiitumainia, naam, wataiharibu kwa upanga.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watayala mazao yenu na chakula chenu; watawamaliza watoto wenu wa kike na wa kiume. Watachinja makundi yenu ya kondoo na ng'ombe; wataiharibu mizabibu yenu na mitini yenu. Miji yenu ya ngome mnayoitegemea, wataiharibu kwa silaha zao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Watayaangamiza mazao yenu na chakula chenu, wataangamiza wana wenu na mabinti zenu; wataangamiza makundi yenu ya kondoo na mbuzi, na ya ng'ombe, wataangamiza mizabibu yenu na mitini yenu. Kwa upanga wataangamiza miji yenye maboma mliyoitumainia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Watayaangamiza mazao yenu na chakula chenu, wataangamiza wana wenu na mabinti zenu; wataangamiza makundi yenu ya kondoo na ya ng’ombe, wataangamiza mizabibu yenu na mitini yenu. Kwa upanga wataangamiza miji yenye maboma mliyoitumainia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao watakula mavuno yako, na mkate wako, ambao iliwapasa wana wako na binti zako kuula; watakula makundi yako ya kondoo na ya ng'ombe; watakula mizabibu yako na mitini yako; wataiharibu miji yako yenye boma, uliyokuwa ukiitumainia, naam, wataiharibu kwa upanga.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watayala mazao yenu na chakula chenu; watawamaliza watoto wenu wa kike na wa kiume. Watachinja makundi yenu ya kondoo na ng'ombe; wataiharibu mizabibu yenu na mitini yenu. Miji yenu ya ngome mnayoitegemea, wataiharibu kwa silaha zao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao watayala mavuno yako na vilaji vyako; watawala hata wanao wa kiume na wa kike, watawala kondoo wako na ng'ombe wako, wataila mizabibu yako na mikuyu yako; wataibomoa kwa panga zao miji yako yenye maboma, uliyoikimbilia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao watakula mavuno yako, na mkate wako, ambao iliwapasa wana wako na binti zako kuula; watakula makundi yako ya kondoo na ya ng’ombe; watakula mizabibu yako na mitini yako; wataiharibu miji yako yenye boma, uliyokuwa ukiitumainia, naam, wataiharibu kwa upanga.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watakula mazao yenu na chakula chenu; watawaua wana na wabinti zenu. Watachinja makundi yenu ya kondoo na ngombe; wataiharibu mizabibu yenu na miti yenu ya matunda ya tini. Miji yenu yenye kuzungukwa na kuta munayoitegemea, wataiharibu kwa silaha zao.