Jeremiah 5:22 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mbona hamniogopi? Nauliza mimi Mwenyezi-Mungu! Kwa nini hamtetemeki mbele yangu? Mimi niliweka mchanga uwe mpaka wa bahari, kizuizi cha daima ambacho bahari haiwezi kuvuka. Ingawa mawimbi yanaupiga, hayawezi kuupita; ingawa yananguruma, hayawezi kuuruka.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Je, haiwapasi kuniogopa mimi?” asema Mwenyezi Mungu. “Je, haiwapasi kutetemeka mbele zangu? Niliufanya mchanga kuwa mpaka wa bahari, kizuizi cha milele ambacho bahari haiwezi kuupita. Mawimbi yanaweza kuumuka, lakini hayawezi kuupita; yanaweza kunguruma, lakini hayawezi kuuvuka.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Je! Hamniogopi mimi? Asema Bwana; hamtatetemeka mbele za uso wangu; mimi niliyeweka mchanga kuwa mpaka wa bahari, kwa amri ya daima, isiweze kuupita? Mawimbi yake yajapoumuka-umuka, hayawezi kushinda nguvu; yajapovuma sana, hayawezi kuupita.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mbona hamniogopi? Nauliza mimi Mwenyezi-Mungu! Kwa nini hamtetemeki mbele yangu? Mimi niliweka mchanga uwe mpaka wa bahari, kizuizi cha daima ambacho bahari haiwezi kuvuka. Ingawa mawimbi yanaupiga, hayawezi kuupita; ingawa yananguruma, hayawezi kuuruka.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Je, haiwapasi kuniogopa mimi?” asema BWANA. “Je, haiwapasi kutetemeka mbele zangu? Niliufanya mchanga kuwa mpaka wa bahari, kizuizi cha milele ambacho haiwezi kupita. Mawimbi yanaweza kuumuka, lakini hayawezi kuupita; yanaweza kunguruma, lakini hayawezi kuuvuka.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Je, haiwapasi kuniogopa mimi?” asema bwana. “Je, haiwapasi kutetemeka mbele zangu? Niliufanya mchanga kuwa mpaka wa bahari, kizuizi cha milele ambacho haiwezi kupita. Mawimbi yanaweza kuumuka, lakini hayawezi kuupita; yanaweza kunguruma, lakini hayawezi kuuvuka.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Je! Hamniogopi mimi? Asema BWANA; hamtatetemeka mbele za uso wangu; mimi niliyeweka mchanga kuwa mpaka wa bahari, kwa amri ya daima, isiweze kuupita? Mawimbi yake yajapoumuka-umuka, hayawezi kushinda nguvu; yajapovuma sana, hayawezi kuupita.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mbona hamniogopi? Nauliza mimi Mwenyezi-Mungu! Kwa nini hamtetemeki mbele yangu? Mimi niliweka mchanga uwe mpaka wa bahari, kizuizi cha daima ambacho bahari haiwezi kuvuka. Ingawa mawimbi yanaupiga, hayawezi kuupita; ingawa yananguruma, hayawezi kuuruka.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mimi hamniogopi, wala uso wangu hamwuzizimukii; ndivyo, asemavyo Bwana. Nami ndimi niwekaye mchanga kuwa mpaka wa bahari, ni tengenezo la kale na kale, nayo haipapiti; ijapo ichafuke, haipashindi, ingawa mawimbi yake yaumuke, hayapapiti.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Je! Hamniogopi mimi? Asema BWANA; hamtatetemeka mbele za uso wangu; mimi niliyeweka mchanga kuwa mpaka wa bahari, kwa amri ya daima, isiweze kuupita? Mawimbi yake yajapoumuka-umuka, hayawezi kushinda nguvu; yajapovuma sana, hayawezi kuupita.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mbona hamuniogopi? –Ni ujumbe wa Yawe.– Kwa nini hamutetemeki mbele yangu? Mimi niliwekea bahari muchanga kuwa mupaka wake; ni kizuizo cha milele ambacho bahari haiwezi kuvuka. Ingawa mawimbi yanaupiga, hayawezi kuupita; ingawa yanavuma, hayawezi kuuruka.