Jeremiah 5:28 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
wamenenepa na kunawiri. Katika kutenda maovu hawana kikomo hawahukumu yatima kwa haki wapate kufanikiwa, wala hawatetei haki za watu maskini.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
wamenenepa na kunawiri. Matendo yao maovu hayana kikomo; hawatetei mashauri ya yatima wapate kushinda, hawatetei haki za maskini.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wamewanda sana, wang'aa; naam, wamepita kiasi kwa matendo maovu; hawatetei madai ya yatima, ili wapate kufanikiwa; wala hawaamui haki ya mhitaji.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
wamenenepa na kunawiri. Katika kutenda maovu hawana kikomo hawahukumu yatima kwa haki wapate kufanikiwa, wala hawatetei haki za watu maskini.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
wamenenepa na kunawiri. Matendo yao maovu hayana kikomo; hawatetei mashauri ya yatima wapate kushinda, hawatetei haki za maskini.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
wamenenepa na kunawiri. Matendo yao maovu hayana kikomo; hawatetei mashauri ya yatima wapate kushinda, hawatetei haki za maskini.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wamenenepa sana, wang'aa; naam, wamepita kiasi kwa matendo maovu; hawatetei madai ya yatima, ili wapate kufanikiwa; wala hawaamui haki ya mhitaji.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
wamenenepa na kunawiri. Katika kutenda maovu hawana kikomo hawahukumu yatima kwa haki wapate kufanikiwa, wala hawatetei haki za watu maskini.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wamenenepa kwa kunona; maneno yao mabaya hupita kiasi; kuamua hawaamui, nao waliofiwa na wazazi hawawaamulii, wawaponye, wala wakiwa hawawakatii mashauri yao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wamewanda sana, wang’aa; naam, wamepita kiasi kwa matendo maovu; hawatetei madai ya yatima, ili wapate kufanikiwa; wala hawaamui haki ya mhitaji.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
wamenenepa na kungaa vizuri. Maovu yao hayana mwisho, hawahukumu yatima kwa kufuatana na sheria kusudi wapate kufanikiwa, wala hawatetei haki za watu wakosefu.