Jeremiah 5:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ee Mwenyezi-Mungu, wewe watafuta daima uaminifu. Umewatwanga, lakini hawakuona uchungu; umewateketeza, lakini walikataa kukosolewa. Wamezifanya nyuso zao kuwa ngumu kuliko mwamba; wamekataa kabisa kurudi kwako.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ee Mwenyezi Mungu, je, macho yako hayaitafuti kweli? Uliwapiga, lakini hawakusikia maumivu, uliwapondaponda, lakini walikataa maonyo. Walifanya nyuso zao kuwa ngumu kuliko jiwe nao walikataa kutubu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ee Bwana, macho yako je! Hayaangalii uaminifu? Umewapiga, lakini hawakuhuzunika; umewakomesha, lakini wamekataa kurudiwa wamefanya nyuso zao kuwa ngumu kuliko mwamba wamekataa kurudi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ee Mwenyezi-Mungu, wewe watafuta daima uaminifu. Umewatwanga, lakini hawakuona uchungu; umewateketeza, lakini walikataa kukosolewa. Wamezifanya nyuso zao kuwa ngumu kuliko mwamba; wamekataa kabisa kurudi kwako.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ee BWANA, je, macho yako hayaitafuti kweli? Uliwapiga, lakini hawakusikia maumivu, uliwapondaponda lakini walikataa marudi. Walifanya nyuso zao kuwa ngumu kuliko jiwe nao walikataa kutubu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ee bwana, je, macho yako hayaitafuti kweli? Uliwapiga, lakini hawakusikia maumivu, uliwapondaponda, lakini walikataa maonyo. Walifanya nyuso zao kuwa ngumu kuliko jiwe nao walikataa kutubu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ee BWANA, macho yako je! Hayaangalii uaminifu? Umewapiga, lakini hawakuhuzunika; umewakomesha, lakini wamekataa kurudiwa wamefanya nyuso zao kuwa ngumu kuliko mwamba wamekataa kurudi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ee Mwenyezi-Mungu, wewe watafuta daima uaminifu. Umewatwanga, lakini hawakuona uchungu; umewateketeza, lakini walikataa kukosolewa. Wamezifanya nyuso zao kuwa ngumu kuliko mwamba; wamekataa kabisa kurudi kwako.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Bwana, kumbe macho yako hayautazami welekevu? Uliwapiga, lakini hawakuzizimuka; ukawapiga tena, lakini wakakataa kuonyeka. Wakazishupaza nyuso zao kupita miamba, wakakataa kurudi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ee BWANA, macho yako je! Hayaangalii uaminifu? Umewapiga, lakini hawakuhuzunika; umewakomesha, lakini wamekataa kurudiwa wamefanya nyuso zao kuwa ngumu kuliko mwamba wamekataa kurudi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ee Yawe, wewe unatafuta uaminifu siku zote. Umewatwanga, lakini hawakuona uchungu; umewateketeza, lakini walikataa maonyo. Wamevifanya vichwa vyao kuwa vigumu kuliko jiwe; wamekataa kabisa kurudi kwako.