Jeremiah 5:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa hiyo simba kutoka msituni atawaua; mbwamwitu kutoka jangwani atawararua. Chui anaivizia miji yao. Kila atokaye humo atararuliwa vipandevipande, kwa sababu dhambi zao ni nyingi, maasi yao ni makubwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo simba wa mwituni atawashambulia, mbwa-mwitu wa jangwani atawaangamiza, chui atawavizia karibu na miji yao, ili kumrarua vipande vipande yeyote atakayethubutu kutoka nje, kwa maana uasi wao ni makubwa, na kukengeuka kwao kumekuwa ni kwingi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, kwa hiyo, simba atokaye mwituni atawaua, mbwa-mwitu wa jioni atawateka, chui ataivizia miji yao, kila mtu atokaye humo atararuliwa vipande vipande; kwa sababu makosa yao ni mengi, na kurudi nyuma kwao kumezidi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa hiyo simba kutoka msituni atawaua; mbwamwitu kutoka jangwani atawararua. Chui anaivizia miji yao. Kila atokaye humo atararuliwa vipandevipande, kwa sababu dhambi zao ni nyingi, maasi yao ni makubwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo simba kutoka mwituni atawashambulia, mbwa mwitu kutoka jangwani atawaangamiza, chui atawavizia karibu na miji yao kumrarua vipande vipande ye yote atakayethubutu kutoka nje, kwa maana maasi yao ni makubwa na kukengeuka kwao kumekuwa ni kwingi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo simba kutoka mwituni atawashambulia, mbwa mwitu kutoka jangwani atawaangamiza, chui atawavizia karibu na miji yao, ili kumrarua vipande vipande yeyote atakayethubutu kutoka nje, kwa maana maasi yao ni makubwa, na kukengeuka kwao kumekuwa ni kwingi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, kwa hiyo, simba atokaye mwituni atawaua, mbwamwitu wa jioni atawateka, chui ataivizia miji yao, kila mtu atokaye humo atararuliwa vipande vipande; kwa sababu makosa yao ni mengi, na kurudi nyuma kwao kumezidi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa hiyo simba kutoka msituni atawaua; mbwamwitu kutoka jangwani atawararua. Chui anaivizia miji yao. Kila atokaye humo atararuliwa vipandevipande, kwa sababu dhambi zao ni nyingi, maasi yao ni makubwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa sababu hii simba wa mwituni amewapiga, naye mbwa wa jangwani akawaangamiza, naye chui huwavizia kwenye miji yao, kila atakayetoka mle araruliwe. Kwani mapotovu yao ni mengi, ukatavu wao ni wenye nguvu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, kwa hiyo, simba atokaye mwituni atawaua, mbwa-mwitu wa jioni atawateka, chui ataivizia miji yao, kila mtu atokaye humo atararuliwa vipande vipande; kwa sababu makosa yao ni mengi, na kurudi nyuma kwao kumezidi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hiyo simba kutoka pori atawaua; imbwa wa pori kutoka jangwa atawararua. Chui anaivizia miji yao. Kila mutu anayetoka humo atararuliwa vipandevipande, kwa sababu zambi zao ni nyingi, maasi yao ni makubwa.