Jeremiah 50:14 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Enyi nyote wapiga mishale stadi, shikeni nafasi zenu kuuzingira mji wa Babuloni; upigeni, msibakize mshale hata mmoja, maana umenikosea mimi Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Shikeni nafasi zenu kuzunguka Babeli, enyi nyote mvutao upinde. Mpigeni! Msibakize mshale wowote, kwa kuwa ametenda dhambi dhidi ya Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Jipangeni juu ya Babeli pande zote, Ninyi nyote mpindao upinde; Mpigeni, msiuzuie hata mshale mmoja; Kwa maana amemtenda Bwana dhambi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Enyi nyote wapiga mishale stadi, shikeni nafasi zenu kuuzingira mji wa Babuloni; upigeni, msibakize mshale hata mmoja, maana umenikosea mimi Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Shikeni nafasi zenu kuzunguka Babeli, enyi nyote mvutao upinde. Mpigeni! Msibakize mshale wo wote, kwa kuwa ametenda dhambi dhidi ya BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Shikeni nafasi zenu kuzunguka Babeli, enyi nyote mvutao upinde. Mpigeni! Msibakize mshale wowote, kwa kuwa ametenda dhambi dhidi ya bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Jipangeni juu ya Babeli pande zote, Ninyi nyote mpindao upinde; Mpigeni, msiuzuie hata mshale mmoja; Kwa maana amemtenda BWANA dhambi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Enyi nyote wapiga mishale stadi, shikeni nafasi zenu kuuzingira mji wa Babuloni; upigeni, msibakize mshale hata mmoja, maana umenikosea mimi Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Jipangeni na kuuzunguka Babeli, ninyi nyote mpindao pindi! Upigeni mishale, msiitendee choyo! Kwani wamemkosea Mungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Jipangeni juu ya Babeli pande zote, Ninyi nyote mpindao upinde; Mpigeni, msiuzuie hata mshale mmoja; Kwa maana amemtenda BWANA dhambi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Enyi wafundi wote wapiga mishale, mujipange kwa kuzunguka muji wa Babeli kwa vita; mupige mishale, musiache mushale hata mumoja, maana umenikosea mimi Yawe.