Jeremiah 50:17 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Israeli ni kondoo wanaowindwa na kufukuzwa na simba. Kwanza waliangamizwa na mfalme wa Ashuru, na sasa Nebukadneza mfalme wa Babuloni, amevunjavunja mifupa yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Israeli ni kundi lililotawanyika ambalo simba wamelifukuzia mbali. Wa kwanza kumla alikuwa mfalme wa Ashuru, wa mwisho kuponda mifupa yake alikuwa Nebukadneza mfalme wa Babeli.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Israeli ni kondoo aliyetawanywa; simba wamemfukuzia mbali; kwanza mfalme wa Ashuru amemla, na mwisho Nebukadreza huyu, mfalme wa Babeli, amemvunja mifupa yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Israeli ni kondoo wanaowindwa na kufukuzwa na simba. Kwanza waliangamizwa na mfalme wa Ashuru, na sasa Nebukadneza mfalme wa Babuloni, amevunjavunja mifupa yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Israeli ni kundi lililotawanyika ambalo simba wamelifukuzia mbali. Wa kwanza kumla alikuwa mfalme wa Ashuru, wa mwisho kuponda mifupa yake alikuwa Nebukadneza mfalme wa Babeli.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Israeli ni kundi lililotawanyika ambalo simba wamelifukuzia mbali. Wa kwanza kumla alikuwa mfalme wa Ashuru, wa mwisho kuponda mifupa yake alikuwa Nebukadneza mfalme wa Babeli.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Israeli ni kondoo aliyetawanywa; simba wamemfukuzia mbali; kwanza mfalme wa Ashuru amemla, na mwisho Nebukadneza huyu, mfalme wa Babeli, amemvunja mifupa yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Israeli ni kondoo wanaowindwa na kufukuzwa na simba. Kwanza waliangamizwa na mfalme wa Ashuru, na sasa Nebukadneza mfalme wa Babuloni, amevunjavunja mifupa yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Waisiraeli ni kama kondoo waliotawanyika kwa kufukuzwa na simba: kwanza mfalme wa Asuri aliwala, mwisho Nebukadinesari, mfalme wa Babeli, aliwavunja mifupa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Israeli ni kondoo aliyetawanywa; simba wamemfukuzia mbali; kwanza mfalme wa Ashuru amemla, na mwisho Nebukadreza huyu, mfalme wa Babeli, amemvunja mifupa yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Israeli ni kama kondoo wanaowindwa na kufukuzwa na simba. Kwanza waliangamizwa na mufalme wa Asuria, na sasa Nebukadneza mufalme wa Babeli, amevunjavunja mifupa yake.