Jeremiah 50:2 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Tangazeni kati ya mataifa, twekeni bendera na kutangaza, Msifiche lolote. Semeni: ‘Babuloni umetekwa, Beli ameaibishwa. Merodaki amefadhaishwa; sanamu zake zimeaibishwa, vinyago vyake vimefadhaishwa.’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Tangazeni! Hubirini katikati ya mataifa, Inueni bendera na mkahubiri; msiache kitu chochote, bali semeni, ‘Babeli utatekwa; Beli ataaibishwa, Merodaki atajazwa na hofu kuu. Sanamu zake zitaaibishwa na vinyago vyake vitajazwa hofu kuu.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tangazeni katika mataifa, Mkahubiri na kutweka bendera; Hubirini, msifiche, semeni, Babeli umetwaliwa! Beli amefedheheka; Merodaki amefadhaika; Sanamu zake zimeaibishwa, Vinyago vyake vimefadhaika.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Tangazeni kati ya mataifa, twekeni bendera na kutangaza, Msifiche lolote. Semeni: ‘Babuloni umetekwa, Beli ameaibishwa. Merodaki amefadhaishwa; sanamu zake zimeaibishwa, vinyago vyake vimefadhaishwa.’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Tangazeni na mhubiri katikati ya mataifa, twekeni bendera na mkahubiri; msiache kitu cho chote, bali semeni, ‘Babeli utatekwa; Beli ataaibishwa, Merodaki atajazwa na hofu kuu. Sanamu zake zitaaibishwa na vinyago vyake vitajazwa hofu kuu.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Tangazeni na mhubiri katikati ya mataifa, twekeni bendera na mkahubiri; msiache kitu chochote, bali semeni, ‘Babeli utatekwa; Beli ataaibishwa, Merodaki atajazwa na hofu kuu. Sanamu zake zitaaibishwa na vinyago vyake vitajazwa hofu kuu.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tangazeni katika mataifa, Mkahubiri na kutweka bendera; Hubirini, msifiche, semeni, Babeli umetwaliwa! Beli amefedheheka; Merodaki amefadhaika; Sanamu zake zimeaibishwa, Vinyago vyake vimefadhaika.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Tangazeni kati ya mataifa, twekeni bendera na kutangaza, Msifiche lolote. Semeni: ‘Babuloni umetekwa, Beli ameaibishwa. Merodaki amefadhaishwa; sanamu zake zimeaibishwa, vinyago vyake vimefadhaishwa.’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yatangazeni kwa mataifa, wayasikie! Twekeni bendera! Yasimulieni, msiyafiche! Semeni: Babeli umetekwa, Beli amepatwa na soni, Merodaki amestuka, vinyago vyao vimeumbuliwa, mifano yao imevunjika!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tangazeni katika mataifa, Mkahubiri na kutweka bendera; Hubirini, msifiche, semeni, Babeli umetwaliwa! Beli amefedheheka; Merodaki amefadhaika; Sanamu zake zimeaibishwa, Vinyago vyake vimefadhaika.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutangaze kati ya mataifa, munyanyue bendera na kutangaza, musifiche jambo lolote. Museme: Babeli umetekwa, mungu Beli amepatishwa haya. Merodaki amefazaishwa; sanamu zake zimefezeheshwa, miungu yake imefazaishwa.