Jeremiah 50:20 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Siku hizo na wakati huo, uovu utatafutwa nchini Israeli, lakini hautapatikana; dhambi itatafutwa nchini Yuda, lakini haitapatikana; maana mimi nitawasamehe wale ambao nimewabakiza. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Katika siku hizo, wakati huo,” asema Mwenyezi Mungu, “uchunguzi utafanyika kwa ajili ya kosa la Israeli, lakini halitaonekana, na kwa ajili ya dhambi za Yuda, lakini haitapatikana hata moja, kwa kuwa nitawasamehe mabaki nitakaowaacha.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Katika siku hizo na wakati huo, asema Bwana, uovu wa Israeli utatafutwa, wala uovu hapana; na dhambi za Yuda zitatafutwa, wala hazitaonekana; maana nitawasamehe wale niwaachao kuwa mabaki.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Siku hizo na wakati huo, uovu utatafutwa nchini Israeli, lakini hautapatikana; dhambi itatafutwa nchini Yuda, lakini haitapatikana; maana mimi nitawasamehe wale ambao nimewabakiza. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika siku hizo, wakati huo,” asema BWANA, “uchunguzi utafanyika kwa ajili ya kosa la Israeli, lakini halitakuwepo, kwa ajili ya dhambi za Yuda, lakini haitapatikana hata moja, kwa kuwa nitawasamehe mabaki nitakaowaacha.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika siku hizo, wakati huo,” asema bwana, “uchunguzi utafanyika kwa ajili ya kosa la Israeli, lakini halitakuwepo, kwa ajili ya dhambi za Yuda, lakini haitapatikana hata moja, kwa kuwa nitawasamehe mabaki nitakaowaacha.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Katika siku hizo na wakati huo, asema BWANA, uovu wa Israeli utatafutwa, wala hakuna uovu; na dhambi za Yuda zitatafutwa, wala hazitaonekana; maana nitawasamehe wale niwaachao kuwa mabaki.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Siku hizo na wakati huo, uovu utatafutwa nchini Israeli, lakini hautapatikana; dhambi itatafutwa nchini Yuda, lakini haitapatikana; maana mimi nitawasamehe wale ambao nimewabakiza. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndivyo, asemavyo Bwana: Siku zile zitakapotimia, manza, Waisiraeli walizozikora, zitatafutwa, lakini zitakuwa haziko, nayo makosa ya Wayuda, lakini hayataonekana, kwani nitayaondoa kwao, nitakaowasaza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Katika siku hizo na wakati huo, asema BWANA, uovu wa Israeli utatafutwa, wala uovu hapana; na dhambi za Yuda zitatafutwa, wala hazitaonekana; maana nitawasamehe wale niwaachao kuwa mabaki.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku hizo na wakati huo, uovu utatafutiwa katika inchi ya Israeli, lakini hautapatikana; zambi itatafutiwa katika inchi ya Yuda, lakini haitapatikana; maana mimi nitawasamehe wale ambao nimewaponyesha. –Ni ujumbe wa Yawe.