Jeremiah 50:26 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Njoni mkamshambulie kutoka kila upande; zifungueni ghala zake za chakula; mrundikieni marundo ya nafaka! Iangamizeni kabisa nchi hii; msibakize chochote!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Njooni dhidi yake kutoka mbali. Zifungueni ghala zake za nafaka; mlundikeni kama lundo la nafaka. Mwangamizeni kabisa na msimwachie mabaki yoyote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Njoni juu yake toka mpaka ulio mbali; Zifungueni ghala zake; Mfanyeni kuwa magofu na kumharibu kabisa; Msimsazie kitu cho chote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Njoni mkamshambulie kutoka kila upande; zifungueni ghala zake za chakula; mrundikieni marundo ya nafaka! Iangamizeni kabisa nchi hii; msibakize chochote!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Njoni dhidi yake kutoka mbali. Zifungueni ghala zake za nafaka; mlundikeni kama lundo la nafaka. Mwangamizeni kabisa na msimwachie mabaki yo yote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Njooni dhidi yake kutoka mbali. Zifungueni ghala zake za nafaka; mlundikeni kama lundo la nafaka. Mwangamizeni kabisa na msimwachie mabaki yoyote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Njooni juu yake toka mpaka ulio mbali; Zifungueni ghala zake; Mfanyeni kuwa magofu na kumharibu kabisa; Msimsazie kitu chochote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Njoni mkamshambulie kutoka kila upande; zifungueni ghala zake za chakula; mrundikieni marundo ya nafaka! Iangamizeni kabisa nchi hii; msibakize chochote!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Njoni huku na kutoka kwenye mapeo ya nchi! Vifungueni vyanja vyake vya ngano, mzikusanye kuwa chungu, kisha zimalizeni kwa kuziteketeza, masao yasipatikane kamwe!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Njoni juu yake toka mpaka ulio mbali; Zifungueni ghala zake; Mfanyeni kuwa magofu na kumharibu kabisa; Msimsazie kitu cho chote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mukuje kumushambulia kutoka kila upande; muzifungue gala zake za chakula; mumulundikie malundo ya ngano! Muiangamize kabisa inchi hii; musiache kitu chochote!