Jeremiah 50:29 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Waiteni wapiga mishale waishambulie Babuloni. Pelekeni kila mtu ajuaye kuvuta upinde. Uzingireni mji pasiwe na yeyote atakayetoroka. Ulipizeni kadiri ya matendo yake yote; utendeeni kama ulivyowatendea wengine, maana kwa kiburi ulinidharau mimi Mwenyezi-Mungu, Mtakatifu wa Israeli.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Waiteni wapiga mishale dhidi ya Babeli, wote wavutao upinde. Pigeni kambi kumzunguka kabisa, asitoroke mtu yeyote. Mlipizeni kwa matendo yake; mtendeeni kama alivyotenda. Kwa kuwa alimdharau Mwenyezi Mungu, yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Waiteni wapiga mishale juu ya Babeli, Naam, wote waupindao upinde; Pangeni hema kumzunguka pande zote; Ili asiokoke hata mtu mmoja wao; Mlipeni kwa kadiri ya kazi yake; Mtendeni sawasawa na yote aliyoyatenda; Kwa sababu amefanya kiburi juu ya Bwana, Juu yake aliye Mtakatifu wa Israeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Waiteni wapiga mishale waishambulie Babuloni. Pelekeni kila mtu ajuaye kuvuta upinde. Uzingireni mji pasiwe na yeyote atakayetoroka. Ulipizeni kadiri ya matendo yake yote; utendeeni kama ulivyowatendea wengine, maana kwa kiburi ulinidharau mimi Mwenyezi-Mungu, Mtakatifu wa Israeli.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Waiteni wapiga mishale dhidi ya Babeli, wote wale wavutao upinde. Pigeni kambi kumzunguka kabisa, asitoroke mtu ye yote. Mlipizeni kwa matendo yake; mtendeeni kama alivyotenda. Kwa kuwa alimdharau BWANA, yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Waiteni wapiga mishale dhidi ya Babeli, wote wale wavutao upinde. Pigeni kambi kumzunguka kabisa, asitoroke mtu yeyote. Mlipizeni kwa matendo yake; mtendeeni kama alivyotenda. Kwa kuwa alimdharau bwana, yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Waiteni wapiga mishale juu ya Babeli, Naam, wote waupindao upinde; Pangeni hema kumzunguka pande zote; Ili asiokoke hata mtu mmoja wao; Mlipeni kwa kadiri ya kazi yake; Mtendeni sawasawa na yote aliyoyatenda; Kwa sababu amefanya kiburi juu ya BWANA, Juu yake aliye Mtakatifu wa Israeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Waiteni wapiga mishale waishambulie Babuloni. Pelekeni kila mtu ajuaye kuvuta upinde. Uzingireni mji pasiwe na yeyote atakayetoroka. Ulipizeni kadiri ya matendo yake yote; utendeeni kama ulivyowatendea wengine, maana kwa kiburi ulinidharau mimi Mwenyezi-Mungu, Mtakatifu wa Israeli.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Waiteni wapiga mishale wote wanaopinda pindi, waje Babeli, wapige kambi zao kuuzunguka, usipate pa kukimbilia. Ulipisheni matendo yake! Yote, uliyoyafanya, ufanyizieni yaleyale! Kwani umejivuna kuwa mkuu kuliko Bwana, kuliko yeye aliye Mtakatifu wa Isiraeli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Waiteni wapiga mishale juu ya Babeli, Naam, wote waupindao upinde; Pangeni hema kumzunguka pande zote; Ili asiokoke hata mtu mmoja wao; Mlipeni kwa kadiri ya kazi yake; Mtendeni sawasawa na yote aliyoyatenda; Kwa sababu amefanya kiburi juu ya BWANA, Juu yake aliye Mtakatifu wa Israeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Muwaite wapiga mishale waishambulie Babeli. Mupeleke kila mutu anayejua kuvuta upinde. Muuzunguke muji kusikuwe mutu yeyote atakayetoroka. Muulipize kadiri ya matendo yake yote; muutendee kama ulivyowatendea wengine, maana kwa kiburi ulinizarau mimi Yawe, Mutakatifu wa Israeli.