Jeremiah 50:34 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini mimi, Mkombozi wao ni mwenye nguvu. Mwenyezi-Mungu wa Majeshi ndilo jina langu. Hakika nitatetea kisa chao ili nilete amani katika nchi yao, lakini taabu kwa wakazi wa Babuloni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini Mkombozi wao ana nguvu; Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni ndilo jina lake. Atatetea shauri lao kwa nguvu ili alete amani nchini mwao, lakini ataleta msukosuko kwa wale wanaoishi Babeli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mkombozi wao ni hodari; Bwana wa majeshi ndilo jina lake; yeye atawatetea kwa bidii, apate kuistarehesha nchi, na kuwasumbua wakaao katika Babeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini mimi, Mkombozi wao ni mwenye nguvu. Mwenyezi-Mungu wa Majeshi ndilo jina langu. Hakika nitatetea kisa chao ili nilete amani katika nchi yao, lakini taabu kwa wakazi wa Babuloni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini Mkombozi wao ana nguvu; BWANA Mwenye Nguvu Zote ndilo jina lake. Atatetea kwa nguvu shauri lao ili kwamba alete raha katika nchi yao, lakini ataleta msukosuko kwa wale waishio Babeli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini Mkombozi wao ana nguvu; bwana Mwenye Nguvu Zote ndilo jina lake. Atatetea kwa nguvu shauri lao ili alete raha katika nchi yao, lakini ataleta msukosuko kwa wale waishio Babeli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mkombozi wao ni hodari; BWANA wa majeshi ndilo jina lake; yeye atawatetea kwa bidii, apate kuistarehesha nchi, na kuwasumbua wakaao katika Babeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini mimi, Mkombozi wao ni mwenye nguvu. Mwenyezi-Mungu wa Majeshi ndilo jina langu. Hakika nitatetea kisa chao ili nilete amani katika nchi yao, lakini taabu kwa wakazi wa Babuloni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini mkombozi wao ni mwenye nguvu, Bwana Mwenye vikosi ni Jina lake. Yeye atawagombea hayo magomvi yao, kusudi aitulize nchi, lakini wakaao Babeli atawahangaisha.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mkombozi wao ni hodari; BWANA wa majeshi ndilo jina lake; yeye atawatetea kwa bidii, apate kuistarehesha nchi, na kuwasumbua wakaao katika Babeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini mimi, Mukombozi wao ni mwenye nguvu. Yawe wa majeshi ndilo jina langu. Hakika nitatetea maneno yao kusudi nilete amani katika inchi yao, lakini taabu kwa wakaaji wa Babeli.